Usambazaji wa Vifaa vya CEmONC, Mikoa ya Dodoma na Singida
Bohari ya Dawa (MSD), kupitia Kanda yake ya Dodoma inayohudumia Mikoa ya Singida na Dodoma imeendelea na zoezi la usambazaji wa vifaa vya huduma ya dharula ya mama na mtoto (Comprehensive Emergency Obstetric and New Born Care Services – CEmONC).
Akizungumzia usambazaji huo Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma Ndg. John Sipendi, amesema usambazaji wa vifaa hivyo kwenyevituo vya kutolea huduma za Afyavinavyohudumiwa na Kanda yake ya Dodoma ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuboresha huduma za dharula za mama na mtoto.
Amebainisha kwamba kwa sasa Kanda yake inatekeleza usambazaji kwenye vituo takribani 26 vya kutolea huduma za afya ambavyo vilianishwa kwa ajili ya kupatiwa vifaa hivyo katika Mikoa ya Singida na Dodoma.
"Ikumbukwe kwamba Rais amekuwa akiweka wazi kuwa moja ya vipaumbele katika serikali ya awamu hii ya 6, ni kuhakikishainaboreshaji huduma, hususani zitakazopunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua". Alisema Sipendi
Meneja Sipendi amesisitiza Kwamba, ataendelea kuhakikisha vifaa vyote vinavyoletwa kutoka makao makuu vinasambazwa kwa wakati na haraka kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoainishwa.
Hata hivyo, pamoja na usambazaji wa vifaa vya CEmONC, Kanda ya Dodoma imeendelea pia na usambazaji bidhaa nyingine za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya takribani 685 vilivyopo katika Mikoa ya Singida na Dodoma.
- Log in to post comments