Skip to main content
Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abuwafa (Kulia) Akikabidhi Msaada wa Vifaa Tiba kwa Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi(Kushoto), Makao Makuu ya Bohari ya Dawa, Jijini Dar es Salaam.

Serikali Ya Misri Yatoa Msaada wa Vifaa Tiba kwa Tanzania

Ubalozi wa Misri nchini Tanzania, leo tarehe 8/9/2022, umetoa msaada vifaa tiba kwa Serikali ya Tanzania, kwa ajili ya kuboresha huduma za afya nchini.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya dola za Kimarekeni elfu 27 (USD 27,000), ambazo ni sawa na takribani shilingi milioni 62.9 za kitanzania, umekabidhiwa rasmi kwa serikali ya Tanzania.

Akikabidhi msaada huo Balozi wa Misri hapa nchini, Mhe. Mohamed Gaber Abuwafa amesema serikali ya Misiri itaendelea na juhudi za kuunga mkono serikali ya Tanzania kuboresha huduma za afya.

"Serikali ya Misri kupitia shirika lake la EAPD, imetoa msaada huu ili kuboresha huduma za afya, ikumbukwe huu sio msaada wa kwanza na wala hautakua wa mwisho, kwani nchi zetu zimekua na uhusiano wa muda mrefu katika nyanja mbalimbali, hivyo mbali na msaada huu, tunatazamia siku zijazo kuazisha ushirikiano katika kubadilishana utaalamu na wataalamu kupitia sekta ya afya”. Alisisitiza Balozi Mhe. Abuwafa

Mhe. Abuwafa ameongeza kuwa Serikali ya Misri inaangalia uwezekano wa kuwekeza nchini kwenye sekta ya viwanda vya dawa na vifaa tiba, ili kuendeleza uhusiano wa muda mrefu baina pande hizo mbili.

"Serikali ya Misri itaendela kusaidia sekta mbalimbali nchini, ikiwemo uanzishaji wa viwanda vya dawa, ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha na kusogeza huduma za afya karibu na jamiii kwa gharama nafuu" Alisema Balozi Abuwafa.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi, ameishukuru Serikali ya Misri kupitia ubalozi wake nchini, kwa kuipatia Tanzania msaada huo, na kusisitiza kwamba utaenda kuwa chachu ya kuboresha afya za wananchi.

"Kwa niaba ya serikali ya Tanzania, tunaipongeza na kuishukuru serikali ya Misri kwa kutupatia msaada huu kwaajili ya kuboresha afya za watanzania na ushirikiano uliopo baina ya mataifa yetu, tunatumaini kwamba huu hautakuwa msaada wa mwisho, bali muendelezo wa ushirikiano zaidi baina ya mataifa yetu." Alisema Msasi

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.