MSD Yatoa Mafunzo kwa Wataalamu wa Vifaa Tiba na Maabara Nchini.
Mafunzo ya siku tatu kwa wahandisi vifaa tiba na wataalam wa Maabara nchini, yamefungwa leo mkoani Morogoro.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa wakati mmoja kwa mikoa mitano kwa ajili ya wataalam wa nchi nzima yalikuwa na lengo la kuwafundisha wataalamu wa usimikaji, matumizi na ukarabati wa mashine za maabara na vifaa vinavyosambazwa na MSD.
Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji Bw.William Singano amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa wahandisi vifaa tiba na wataalam wa maabara kwa kuwa yanawawesha watumiaji hao kumudu kuzitumia, kuzitunza na kuzifanyia ukarabati.
BW. Singano ameishuikuru Serikali kuboresha huduma za afya kwa kuwezesha mashine na vifaa vya kisasa nchi nzima. Mafunzo hayo yalitolewa mikoa ya Tabora, Morogoro, Mbeya, Kilimanjaro na Mwanza ambapo wataalam kutoka mikoa mingine yote waliungana kupata mafunzo hayo kwa pamoja.
- Log in to post comments