MSD Yateta na Wazalishaji wa Ndani wa Bidhaa za Afya.
#DAR ES SALAAM
Wazalishaji wa ndani wa bidhaa za afya wamehakikishiwa soko la ndani na nje la bidhaa wanazozalisha, huku wakisisitizwa kuzingatia kiasi cha mahitaji na ubora wa bidhaa hizo.
Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Wazalishaji wa ndani wa bidhaa za afya ulioandaliwa na Bohari ya Dawa (MSD) Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi amesema kuwa serikali ina dhamira ya kuwawezesha wazalishaji wa ndani hasa katika masuala ya sheria na taratibu zinazohusiana na viwanda vya bidhaa za afya.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Leopord Shayo ameeleza kuwa kwa sasa MSD inaagiza zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa za afya nje ya nchi,hali inayochangia kutumia fedha nyingi za kigeni.
Ameeongeza kuwa, nchi itaweza kukabiliana na majanga pindi yanapotokea, kuwa na uhakika wa ubora wa bidhaa za afya na kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bishaa za afya kwa wakati.
Mbali na wazalishaji hao,mkutano huo ulihusisha wadau wengine wanaofanya kazi karibu na MSD ambao ni pamoja na Wizara ya Afya Taasisi ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),PPRA, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) sambamba na Ofisi ya Msajili wa Ha zina
Lengo la mkutano huo ni wadau hao kukaa pamoja na kuangalia namna ya kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya kutoka kwa wazalishaji wa ndani.
Aidha kikao hicho pia kililenga kutathimini mahitaji ya bidhaa za afya nchini, sambamba na ubora wake
- Log in to post comments