Skip to main content
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius M. Emmanuel(Aliyeko Katikati Mstari wa Mbele) Akiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Uzinduzi wa Usambazaji Vyandarua Wilayani Kongwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Atoa Rai - Matumizi ya Vyandarua

Kongwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius M. Emmanuel amewataka wakazi na wazazi wote wilayani humo kutumia vyema na kwa lengo lililokusudiwa vyandarua vya msaada wanavyopatiwa serikali, ili adhima ya serikali ya kupambana na ugonjwa wa Malaria iweze kutimia.

Mhe. Remidius ametoa rai hiyo hii leo wakati akizindua rasmi zoezi la usambazaji wa vyandarua mashuleni wilayani humo, linalofanya na Bohari ya Dawa (MSD).

"lengo serikali kuwagawia vyandarua ni kuwakinga watoto wetu dhidi ya ugonjwa hatari wa Malaria, hivyo naomba vitumike kama ilivyokusudiwa na kwa matumizi ambayo ni kinyume na matakwa ya lengo la serikali kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria. Alisema Mhe. Remidius.

Kwa upande wake Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma, Bw. John Sipendi amesema MSD imejipanga vizuri kusambaza vyandarua kwenye shule zote zilizoainishwa na kwa muda uliopangwa.

" Sisi kama MSD tumejipanga kuhakikisha tunatekeleza zoezi hili la usambazaji kwa ufanisi na kwa wakati, hivyo niwatoe hof kwani hakuna shule itakosa vyandarua.

Bw. Sipendi ameongeza kuwa tayari magari ya usambazaji yako wilayani humo, na jumla ya vyandarua 87,038 vitasambazwa kwenye shule za msingi 123.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.