Skip to main content
Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu Akiwa kwenye Picha ya Pamoja na Wajumbe Wapya wa Bodi ya                Wadhamini ya MSD, Mara baada ya Kuitambulisha Mbele ya Waandishi wa Habari.

Mhe. Ummy Mwalimu Azindua Bodi Mpya ya Wadhamini ya MSD.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amezindua Bodi mpya ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuwaelekeza wajumbe hao Bodi kuhakikisha wanawezesha kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya zenye ubora na bei nafuu.

 Waziri Ummy amewaeleza wajumbe hao wa Bodi ya Wadhamini kuwa watapimwa kwa kuangalia hali halisi ya upatikanaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

 Pia, amewasisitiza kuhakikisha katika majukumu yote ya MSD wanazingatia sheria, kanuni na taratibu zote za ununuzi wa umma, ili kuleta ufanisi na tija katika utendaji, sambamba na kuondoa hoja za ukaguzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bi. Rosemary Silaa amewataka watumishi wa MSD kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, ili kubadili taswira iliyojengeka juu ya utendaji usioridhisha wa taasisi hiyo.

 Wajumbe hao ni pamoja na Bi.Rosemary Silaa ambaye ni Mwenyekiti, Dkt. Julius Mwaiselage, Dkt.Ntuli Kapologwe, Meshack Anyingisye, Rehema Katuga, John Mathew Mnali, Dkt. Mwamvita Kissiwa, Dkt. Danstan Hipolite Shewiyo na Brenda Msangi.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.