Maduka ya Dawa ya MSD
Katika kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kusogeza huduma karibu na vituo vya kutolea huduma za afya na kwa wananchi, MSD ilianzisha kimkakati maduka (6) ya dawa (MCOs) kwenye maeneo mbalimbali nchini. Maduka haya ya dawa yalianzishwa kupitia Mpango Mkakati wa Muda wa Kati wa miaka sita (MTSP II) 2014-2020 ambao baadaye ulifanyiwa mapitio mwaka 2017.
Maduka hayo (5) yanapatikana sehemu mbalimbali nchini ambazo ni pamoja na Duka la MSD Mkoani Katavi; Duka la MSD Ruangwa- Mkoani Lindi; Duka la MSD Chato- Mkoani Geita; na Duka la MSD Mkoani Mbeya.
Maduka haya ya Dawa ya MSD (MCO's) yalilenga kupanua na kuboresha kuboresha utoaji wa huduma za afya na kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba karibu na jamii. Maduka haya huuza dawa aina mbalimbali kwa jumla na rejareja kwa kiasi na gharama ambayo jamii inamudu.
Maduka haya hufanya kazi kitaalamu siku saba za wiki kwa kutoa dawa mbalimbali ambazo zimesajiliwa na kuidhinishwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa vya Tiba Tanzania (TMDA). Maduka haya hutumia hazina yake inayozunguka kama mtaji ili kukidhi gharama za uendeshaji wa kila siku.