Huduma za Udhibiti Ubora
Mifumo ya Usimamizi na Michakato ya Utendaji ya Bohari ya Dawa imeidhinishwa na Shirika la Viwango la Kimataifa na kupata ithibibati ya kimataifa ya ISO 9001:2015. Mifumo yote na michakato ya kiutendaji hufanyiwa tathmini, kaguzi na mapitio ya mara kwa mara. Mifumo hii ya udhibiti ubora, inahusisha mchakato wa hatua za udhibiti wa utendakazi, mabadiliko, uhakiki, usimamizi wa vihatarishi na mchanganuo wa takwimu. Wateja wetu wakuu wameona mifumo hii ikiboreshwa na kuleta manufaa na tija katika kipindi ilichopata huduma na MSD.
Usimamizi wetu wa mchakato na mifumo ya udhibiti (QMS) huhakikisha mahitaji ya vifaa, rasilimali, mchakato wa udhibiti, mifumo ya tehama, usimamizi wa ubora, shughuli za ghalani, huduma kwa wateja, akaunti muhimu, wadaiwa, wadai, vihatarishi, usalama, rasilimali watu na mahitaji ya mteja yanasimamiwa na kuboreshwa kwa kiwango cha kimataifa. Kiwango cha ukaguzi binafsi wa hiari, unaoratibiwa na udhibiti ubora wa ndani ni uti wa mgongo wa kuhakikisha michakato inatii na kutumika kama nyenzo ya ukaguzi wa mara kwa mara.
Udhibiti wa vihatarishi ni mchakato muhimu ambao unahakikisha inazuia uwezekano wowote wa kutokea athari, huku kumbukumbu na hatua za kukabiliana na vihatarishi zinawekwa ili kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza. MSD ina Kitengo cha Udhibiti Ubora ambacho kinahakikisha viwango bora vya utoaji huduma vinadumishwa wakati wote wa utendaji kazi. Dharura na hatari kwa vifaa muhimu imetekelezwa, vifaa vya kuhifadhi nakala hujaribiwa kwa msingi uliopangwa. Tathmini za vihatarishi (Udhibiti wa Hasara) hufanywa, matokeo yanachunguzwa, hatua kuchukuliwa na kufungwa.
Juhudi mbalimbali za maboresho zinazoendelea zimesaidia mchakato mzima wa utendakazi na mifumo thabiti ya udhibiti, ilihali mpango wa mafunzo ya ndani umehakikisha kuwa uelewa wa mchakato na uelewa wa waendeshaji unaonekana katika vituo vyetu vyote kiutendaji.