Bodi ya Wadhamini MSD, Yaridhishwa Usambazaji wa Vifaa Tiba Kuwezesha Uzazi Pingamizi kwa Mama na Mtoto
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini MSD Dkt. Ritah Mutagonda, ambaye amefanya ziara kwa wateja wanaohudumiwa na Kanda ya Kilimanjaro, amefurahishwa na utekelezaji wa usambazaji wa vifaa vya kisasa vya kuwezesha uzazi pingamizi kwa mama na mtoto.
Mjumbe huyo ea Bodi ameyasema hayo walipotembelea kituo cha afya Uru Kyaseni, ambapo pamoja na mambo mengine amesema kwa serikali kupitia MSD kuwezesha usambazaji wa vifaa hivyo kunapunguza idadi ku wa ya wagonjwa kufuata huduma hizo hospitaki ya Wilaya na ya rufaa ya mkoa.
Naye Mganga Mfawidhi wa kituo hicho cha Afya Emmanuel Makundi amesema kwa sasa kituo hicho kina toa huduma za kutunza miili, upasuaji na hata huduma za kinywa na meno, ambazo awali hazikuwepo.
Ameongeza kuwa hali ya upatikanaji wa bidhaa za afyakatika kituo hicho kwa sasa ni asilimia 90, na kuomba kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya, ili kuwapunguzia kwenda kununua nje ya MSD.
Ziara hiyo ya Ujumbe wa Bodi na Menejimenti ya MSD kwenye Kanda ya MSD Kilimanjaro, inakuja ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya miaka 30 ya MSD, ambapo MSD inatembelea wateja wake kwenye Kanda zake zote, kwa lengo la kupata mrejesho wa huduma mbalimnbali zitolewazo na MSD.
Kanda ya MSD Kilimanjaro kiutendaji inahudumia vituo vya kutolea huduma za afya, vilivyoko kwenye Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
- Log in to post comments