Mkurugenzi Mkuu MSD, Afanya Mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu PPRA
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Mavere Ali Tukai, amefanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) Bw. Eliakim C. Maswi, juu ya namna bora ya kuboresha ununuzi wa bidhaa za afya, kufuatia changamoto kadhaa zinazoikabili Bohari ya Dawa kwenye eneo hilo.
Mavere amemuelezea Afisa Mtendaji Mkuu huyo mtazamo wake juu ya ununuzi kwenye nyanja mbalimbali kama vile sheria, taratibu, miongozo pamoja na mfumo wa TANEPS.