MSD Kanda ya Mbeya, Yateta na Wafamasia Kuboresha Huduma
MBEYA:
MSD Kanda ya Mbeya imefanya kikao na wafamasia kutoka halimshauri 17 na wafamasia wa mikoa yote inayohudumiwa na Kanda hiyo
Kwa upande wake Meneja wa MSD Kanda ya Mbeya Bw. Marco Masala amesema lengo la kikao hicho ni kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha huduma za upatikanaji wa bidhaa za afya katika mikoa hiyo, pamoja na kuimarisha uhusiano.
Pamoja na mambo mengine kupitia kikao hicho wamekubaliana kuunda kamati maalum ya kudumu itakayosaidiana na Kanda ya MSD Mbeya kufuatilia utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye kikao hicho.
Naye mwenyekiti mteule wa Kamati hiyo Bi. Lucia Mkumbo (Mfamasia wa Mkoa wa Mbeya) ameipongeza MSD kwa kufanikisha kikao hicho na kusema kuwa wapo tayari kufanya kazi kwa kushirikiana ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa, ikiwa ni pamoja na kusimamia na kuhakikisha kuwa vituo vya afya vinaleta maombi ya mahitaji yao mapema na kutumia vyanzo vingine vya mapato badala ya kutegemea fedha inayotoka Serikali kuu pekee.
Hivi karibuni MSD kupitia mipango yake mbalimbali, imejidhatiti kuhakikisha inaimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini, sambamba na kuboresha mawasiliano na mahusiano na wateja na wadau wake
- Log in to post comments