Skip to main content
  • MSD Yaboresha Huduma za Kusafisha Damu- Hospitali ya Tumbi

    PWANI

    Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani - Tumbi imeanza kutoa huduma mpya ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo. Huduma hii imeanza kutolewa baada ya Bohari ya dawa (MSD) kukamilisha usimikaji wa  mashine za kisasa 10 za kusafisha damu, baada ya hospitali ya rufaa ya Tumbi kuboresha miundombinu ya kuwezesha huduma hiyo kupatikana.

    Hatua hiyo ni muendelezo wa maboresho ya huduma za afya nchini yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Afya.

  • Mkuu wa Mkoa wa Njombe Atembelea Kiwanda cha MSD-Idofi

    NJOMBE

    Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Antony Mtaka na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Njombe imetembelea kiwanda cha Bohari ya Dawa (MSD) cha kuzalisha mipira ya mikono kilichopo Idofi, Makambako ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 70.

    Mhe.Mtaka amesema kiwanda hicho ni muhimu kwa sekta ya afya kwani kitapunguza matumizi ya fedha za kigeni kununua bidhaa hiyo nje ya nchi na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa mipira ya mikono nchini.

  • MSD Yapokea Shehena ya Vipimo vya UKIMWI na Kaswende

    Katika kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani MSD imeendelea kupokea na kusambaza bidhaa mbalimbali za afya za kupambana na kudhibiti maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Pamoja na Kaswende.

    Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai ameeleza kuwa miongoni mwa bidhaa za afya ambazo kwa sasa inauhitaji mkubwa na inaendelea kusambazwa na MSD kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ni vipimo vya kupima maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na gonjwa la zinaa la Kaswende (HIV/ Syphilis Duo).

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Atangaza Neema Sekta ya Afya Nchini

    WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa kuwezesha upatikanaji wa wataalam, dawa, vitendanishi na vifaa tiba.

  • Katibu Mtendaji SADC Atembelea MSD

    DAR ES SALAAM: 

    Katibu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)  Mhe. Elias Mpedi Magosipamoja na ujumbe wake, wametembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), yaliyokoKeko jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujionea jinsi taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake sambamba na kupokea mrejesho wa maendeleo ya utekelezaji wa mpango wa manunuzi ya pamoja (SPPS) kwaajili ya nchi wanachana.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.