Skip to main content
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Mkurgenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai(wapili kushoto), na Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Togolani Edriss Mavura (wakwanza kulia) Wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Kiongozi wa Serikali ya Jimbo la Chungcheongbuck   nchini Korea kusini.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Atangaza Neema Sekta ya Afya Nchini

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa kuwezesha upatikanaji wa wataalam, dawa, vitendanishi na vifaa tiba.

Mheshimiwa Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Oktoba 26, 2022 baada ya kushuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) na Serikali ya Jimbo la Chungcheongbuck nchini Korea kusini.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, ambalo pia lilihudhuriwa na Gavana wa jimbo la Chungcheongbuck, Mheshimiwa Majaliwa amesema “Tukio hili la utiaji saini wa makubaliano haya ni ishara kwamba sasa tunakwenda kuimarika kwenye sekta ya dawa, mkataba huu kwetu ni muhimu kwa kuwa tunahitaji kujiimarisha katika eneo la upatikanaji wa dawa na tafiti.”

Sehemu ya makubaliano katika mkataba huo ni kujadili na kuendeleza mahusiano ya kibiashara katika nyanja za masoko ya bidhaa zinazozalishwa na Makampuni ya dawa katika jimbo hilo.

Maeneo mengine ni kubadilishana watumishi, semina za pamoja za wataalamu wao katika nyanja mbalimbali, kubadilishana na kupeana taarifa za uwekezaji kwenye sekta ya dawa, msaada wa kitaalamu na wataalam.

Mheshimiwa Majaliwa alimueleza Gavana huyo kuwa, kutokana na mpango wa Serikali wa kuendelea kuimarisha eneo la utoaji huduma za afya, Serikali ya Tanzania inawakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kujenga viwanda vya dawa na vifaa tiba ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa dawa na vifaa tiba.

Ameupongeza uongozi wa MSD kwa hatua kubwa uliopiga katika mpango wa manunuzi ya pamoja, huku akiahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na MSD, ili kuleta tija na msukumo wa manunuzi ya pamoja ya bidhaa za afya kwa nchi wanachama.

Hatahivyo; ameitaka MSD kuongeza nguvu na ubunifu ili kuvutia nchi nyingi zaidi na kuhakikisha kwamba lengo linafikiwa, huku akipongeza mpango wa kutoa kipaumbele kwa wazalishaji wa ndani, kwani utainua uchumi wa nchi wanachama pamoja na kuongeza ajira.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.