Skip to main content

Tunafanya nini

Bohari ya Dawa (MSD) ni idara inayojitegemea chini ya Wizara ya Afya (MoH), iliyoanzishwa mwaka 1993 kwa Sheria ya Bohari ya Dawa, Sura. 70.Mwaka 2020 sheria ya MSD ilifanyiwa marekebisho na kuifanya MSD kuwa na  majukumu makuu manne ambayo ni Uzalishaji, Ununuzi, Uhifadhi na Usambazaji wa bidhaa za afya kwa ajili ya  vituo vya kutolea huduma za afya vya umma zaidi ya 7,600 nchi nzim na baadhi vya binafsi vilivyoidhinishwa na Wizara ya Afya.

Hivyo MSD inajukumu la kuandaa, kutunza na kusimamia mfumo bora na wa gharama nafuu za ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa dawa na vifaa tiba vinavyohitajika kwa matumizi ya vituo vyote vya afya vya umma. Karibu asilimia 85 ya bidhaa zote za afya za MSD zinanunuliwa kutoka nje ya nchi.

Bohari ya Dawa ina Kanda kumi (10) ambazo zimewekwa kimkakati. Kanda hizo ni pamoja na Dar es Salaam, Mbeya, Iringa, Tabora, Dodoma, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro, Tanga na  Mtwara. Halikadhalika, MSD inaendesha Maduka Matano (5) ya kijamii yaliyokusudiwa kusogeza huduma za bidhaa za afya kuwa karibu na jamii.

Maduka haya yanapatikana katika maeneo yafuatayo; Geita (Chato), Lindi (Ruangwa), Katavi (Mpanda), Arusha (Mlima Meru), na Mbeya. MSD inasambaza bidhaa za afya moja kwa moja kwenye vituo vya afya na usambazaji huu hufanyika kila baada ya miezi miwili.

Kanda za MSD husambaza bidhaa za afya moja kwa moja hadi kwa mteja, na kukabidhi bidhaa hizo, mbele ya Kamati ya Afya ya kituo husika. Usambazaji huo hufanyika kila baada ya miezi miwili kwa kufuata kalenda ya usambazaji.

Modern Warehouse

Mbeya WiB, Mbeya

The Modern Warehouse-in-a Box [WiB] infrastructures with modern working tools across the country have pushed MSD to Centre of Excellence [CoE]. The WiB are constructed using international standards, which enable MSD to have ultra-modern warehouses with vast storage space.

Modern Fleet

MSD Fleet, Modern Fleet

MSD recognizes the importance of basic logistics and transportation infrastructures. MSD ensures that its modern fleets are excellently maintained and operated. MSD's highly motivated team of distribution whose bedrock of the Mission led to a change of distribution strategy to Direct Delivery.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.