Skip to main content

Mfumo wa Usambazaji.

USAMBAZAJI.

Mnyororo wa usambazaji wa Bohari ya Dawa huanzia kwenye maghala yaliyopo Makao Makuu Dar es Salaam, kisha bidhaa husika hupelekwa kwenye Kanda zilizopo kimkakati maeneo mbalimbali nchini na huishia kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya. MSD ina jumla ya magari 215 ya usambazaji, ambayo husambaza dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara moja kwa moja hadi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya  zaidi ya 7,600 nchi nzima. (hospitali, vituo vya Afya na zahanati).

Mfumo wa usambazaji bidhaa za afya moja kwa moja hadi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini, umeleta mapinduzi na maboresho makubwa katika utoaji wa huduma kwa wakati, usambazaji, ubora na utunzaji nyaraka na kumbukumbu husika, hatua iliyopelekea kuridhika kwa wateja. Kanda za MSD, ziko kimkakati katika maeneno mbalimbali nchini ambayo ni pamoja na Dar es salaam, Mtwara, Mbeya, Iringa, Dodoma, Tabora, Mwanza, Kilimanjaro, Tanga pamoja na Kagera.

Wateja wa MSD huwasilisha mahitaji yao kupitia mfumo wa Kusimamia Usafirishaji wa kieletroniki unaofahamika kama Electronic Logistics Management System (eLMIS). Mfumo wa eLMIS umeunganishwa na mfumo wa Epicor unaotumiwa na MSD kuandaa mahitaji ya wateja. MSD pia husambaza bidhaa za Miradi Misonge ambazo mfumo wake wa usambazaji umeunganishwa na bidhaa maalum kwa msaada wa mfumo wa Kusimamia Usafirishaji wa Kielektroniki (ELMIS).

Wadau hawa ni pamoja na Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP), Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), Maendeleo ya Kinga na Chanjo (IVD), Mpango wa Kitaifa wa Kifua Kikuu/Ukoma (NTLP), Magonjwa ya Kitropiki Yaliyosahaulika (NTD), Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCHS) na Kituo cha Chakula na Lishe Tanzania (TFNC). Hatua hii ya kushirikiana na MSD inalenga kupunguza gharama za usambazaji na usimamizi thabiti wa bidhaa za matibabu ndani ya mnyororo mmoja wa ugavi, hivyo kurahisisha usambazaji na ufanisi zaidi. Mfumo huu wa eLMIS pia hutumiwa na Wizara ya Afya na wadau wengine kufuatilia uagizaji, usambazaji na matumizi ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara nchini.

MSD pia ni wasambazaji wa  bidhaa za mnyororo baridi. Bidhaa hizo za mnyororo baridi ni pamoja na  na chanjo na baadhi ya dawa ambazo pia husambazwa kwa zaidi ya vituo 7,600 vya kutolea huduma za afya nchini. Shughuli hii hufanyika kwa kuzingatia miongozo elekezi (SOPs) inayohusisha upokeaji, uhifadhi, upakiaji, usambazaji na makabidhiano kwa wateja wetu. Watumishi wote wa MSD  hupata mafunzo ya kina ya miongozo ya utendaji ambayo huhuishwa kila mwaka kulingana na mahitaji au mabadiliko yanapotokea.

Huduma tunazotoa zinafuata miongozo ya kukidhi viwango vya ubora wa Kimataifa, nidhamu ya viwango vya juu na ubobezi katika usambazaji vinaifanya MSD kuwa ya kipekee kwani michakato  yote huzingatia kanuni za Kimataifa za Usambazaji Bora zilizowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Dawa na Vifaa vya Tiba (TMDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.