Skip to main content

Manunuzi ya Pamoja ya SADC

Kuhusu SPPS

SPPS ni mpango unaojumlisha manunuzi ya pamoja ya bidhaa za afya kwa nchi Wanachama wa SADC kupitia bei zilizojadiliwa na masharti ya uwasilishaji na watengenezaji. Mchakato wa manunuzi kupitia SPPS huanza na nchi Wanachama wa SADC kubainisha mahitaji yao, kisha MSD hutangaza zabuni na kushiriki orodha ya bei, ambapo nchi Wanachama huchagua bidhaa za kununuliwa na kuwasilisha maombi yao.

Mpango wa ugavi huundwa ambapo nchi Wanachama hufahamishwa kuhusu jumla ya thamani na ratiba za akiba na uwasilishaji/usambazaji. Michakato mingine ya ununuzi inafanywa kwa kuzingatia miongozo ya SPPS.

Utekelezaji wa Mradi wa SADC Kupitia MSD

Mnamo mwaka 2017, Mawaziri wa Afya wa SADC na Mawaziri wanaohusika na VVU na UKIMWI wakati wa mkutano wao wa kikanda uliofanyika mwezi Novemba huko Polokwane - Afrika Kusini, waliidhinisha Tanzania kupitia MSD kushughulikia huduma za manunuzi za pamoja (SPPS) za bidhaa za afya kwa nchi 16 wanachama wa SADC. Nchi hizo wanachama zina wastani wa watu milioni 346.

Ofa hiyo iliwasilishwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Februari 2018 na mnamo tarehe 9 Oktoba 2018, Sekretarieti ya MSD na SADC zilitia saini makubaliano kama hatua ya kwanza ya kufanya kazi kwa mpango wa SPPS. MSD ilianzisha Ofisi maalum ya ndani inayohusika na huduma za manunuzi ya SADC na shughuli zake zilianza rasmi Januari 2019.

Sababu kuu ya MSD kuteuliwa kusimamia SPPS ilitokana na uimara na umadhubuti wa mtandao wake wa usambazaji ulioimarishwa vizuri na vifaa vya kisasa vya mnyororo baridi, sambamba na uwezo wake wa uhifadhi wa bidhaa za afya iliyounganishwa na mifumo ya tehama ili kuhakikisha shughuli za ugavi zinawianishwa katika MSD yote.

Nchi Wanachama wa SADC

  • Angola
  • Botswana
  • Comoros
  • DRC
  • Eswatini
  • Lesotho
  • Madagascar
  • Malawi
  • Mauritius
  • Mozambique
  • Namibia
  • Seychelles
  • South Africa
  • Tanzania
  • Zambia
  • Zimbabwe

 

Majukumu ya MSD Kupitia SPPS.

Jukumu kuu la MSD kupitia SPPS ni kuratibu huduma zote za ununuzi wa SADC katika kanda ya SADC, ikijumuisha;

(a) Kutekeleza, kufuatilia, kusaidia na kusimamia huduma za manunuzi ya kielektroniki ya bidhaa za afya kwa kanda ya SADC;

(b) Kusaidia uendelevu wa shughuli za ununuzi wa Dawa na usimamizi wa mnyororo wa ugavi katika Kanda ya SADC;

(c) Kuratibu upashanaji wa taarifa na wazalishaji na nchi wanachama wa SADC

(d) Kuboresha uzalishaji na uwezo wa viwanda vya uzalishaji vilivyopo kikanda;

(e) Kuvutia wawekezaji wapya katika nchi za SADC,

(f) Kuhimiza utangamano wa Kikanda na ajenda ya viwanda

(g) Kuwezesha unafuu wa gharama katika manunuzi na kuboresha upatikanaji wa bidhaa.

(h) Kufanya shughuli nyingine yoyote inayohitajika ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu na bidhaa za afya.

Mafanikio Muhimu ya MSD Kupitia SPPS

Tangu kuanzishwa kwa ofisi ya SADC Pooled Procurement Services. Baadhi ya mafanikio ambayo MSD imepata ni pamoja na:

i.) Kuundwa kwa Miongozo ya SPPS na Mfumo wa Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi;

ii. Kuitisha na kuendesha mkutano wa kitaalamu wa SADC Pooled Procurement wa kikanda mwaka 2019 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwezesha kubadilishana taarifa;

iii. Kutengeneza mfumo kielektroniki (e-SPPS) ili kushughulikia miamala yote ya usimamizi wa ugavi wa SPPS ndani ya eneo;

iv. Kuwezesha kusaini mikataba 41 na watengenezaji wa bidhaa za afya;

v. Kukuza uelewa juu ya matumizi ya mfummo wa SPPS kwa kufanya mikutano na Mabalozi wa SADC walioidhinishwa na Tanzania na nchi za SADC;

 

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.