Skip to main content

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na UKIMWI Yaridhishwa na Utendaji wa MSD.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI imesema  imeridhishwa na hali ya utendaji wa Bohari ya Dawa(MSD) na mipango ya utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo uzalishaji wa dawa ili kupunguza kununua dawa nje ya nchi. 

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Afya na Maswala ya UKIMWI, Mhe. Stansilaus Nyongo baada ya kupokea taarifa ya hali ya utendaji na majukumu ya Bohari ya Dawa (MSD), ambapo ameichagiza MSD kuongeza ufanisi, ubunifu wa hali ya juu kwa kuhakikisha bidhaa za afya zinakuwa toshelevu na  kusambazwa.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti ameshauri MSD kufuatilia na kukusanya madeni ili kuhakikisha inajiendesha vizuri bila kuathiri mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya na kuongeza kuwa wataendelea kuishauri serikali kuiwezesha MSD kupata mtaji ili iweze kujiendesha.

“Bohari ya dawa sasa imeongezewa jukumu moja la kuzalisha bidhaa za afya na kuifanya sasa kutekeleza majukumu manne ambayo ni kuzalisha, kununua, kutunza na kusambaza bidhaa za afya katika vituo vya  vyote vya umma vya kutolea huduma za afya nchini”_  ameeleza  Mhe. Nyongo.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai  kwa uongozi imara katika taasisi hiyo na kuwezesha upatikanaji wa bidhaa za afya kuongezeka na kufikisha vituoni kwa wakati.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai  ameeleza kuwa tayari wameanzisha kampuni Tanzu  ambayo itaingia mikataba na makampuni binafsi ya ndani na nje kuwekeza kwenye  viwanda vya kuzalisha  bidhaa mbalimbali za afya nchini, na wajumbe wanne wa Bodi wa kampuni hiyo tanzu wameshateuliwa.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.