Skip to main content
Meneja wa MSD Kanda ya Kagera Akichangia Mada, Wakati wa Kikao cha Wadau na Wateja wa Kanda hiyo

Wafamasia na Wataalamu wa Maabara Nchini, Waaswa Kuzingatia Wajibu Wao

Wafamasia na Wataalamu wa Maabara Kanda ya Kagera wametakiwa kutambua moyo wa sekta ya afya uko katika upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na kwamba kuhakikisha bidhaa hizo hazikosi katika vituo vya kutolea huduma.

Hayo yamesemwa na Mganga mkuu wa Hospitali ya mkoa wa Geita Omary Sukari kwenye kikao cha majadiliano cha hali ya upatikanaji wa bidhaa za Afya kwa kanda ya kagera inayojumuisha wilaya ya Saba za mkoa kagera na wilaya tatu za Geita.

Sukari alisema,mchakato wa upatikanaji wa bidhaa hizo unaanzia kwa wataalamu kwa kuanza kufanya makadilio kila unapoanza mwaka wa fedha serikalini.

Alisema kuna kila hali ya kuangalia bidha gani ipo kwa kiwango chenye kutosheleza,au iko chini na wingi upi haitumiki na kutojulikana matumizi yake na kufanya dawa kuisha muda.

"Ngazi ya vituo ifanye hiyo na kote hadi mkoa kwenda wizarani hadi kufikia kupelekwa kwa wenzetu wa MSD ambao wanapelekewa oda zinazotakiwa"alisema Sukari.

Aidha alisema kituo kikiwa na bidhaa hufanya mtejaa akitoka kwenye huduma afarijike kulingana na huduma aliyopata kupitia vifaa tiba.

"Hakuna mteja atakayetoka kwenye kituo cha Afya kama uhitaji wa tiba yake utakuwa haujatosheleza ata kama utakuwa umemfanyia kitu gani"alisema Sukari.

Meneja wa Bohari ya dawa kanda ya kagera (MSD) Kalendero Masatu alisema,yapo mategemeo ya kuwa na ongezeko la upatikanaji wa dawa kwa asilimia 70hadi 80.

Alisema,tangu mwezi julai mwaka jana hadi kumalizika mwezi June 30mwaka huu,upatikanaji wa dawa uliongezeka kwa asilimia 65kwenye robo ya nne kutoka 55 robo ya kwanza.

Aliongeza kuwa ongezeko hilo lilifanya kuwa na asilimia 90ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za Afya ambazo hufanya oda na (MSD)watoa huduma ambao ni wafamasia na wataalamu wa maabara.

"Na jambo hilo hufanya kuwa na mnyororo wa ugavi ulio Bora katika utowaji wa vifaa tiba kwenye vituo vya Afya na kwa kanda yetu hii ya kagera yenye mikoa miwili ambayo ni Kagera yenyewe na Geita kwa baadhi ya wilaya"alisema Masatu.

Alisema, oda zinatolewa kulingana na uhitaji wa mteja katika kituo chake,ambacho anafahamu kulingana na makadilio na kusaidia sawa zisiweze kuosha muda wake.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.