MSD Yaboresha Huduma za Kusafisha Damu- Hospitali ya Tumbi
PWANI
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani - Tumbi imeanza kutoa huduma mpya ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo. Huduma hii imeanza kutolewa baada ya Bohari ya dawa (MSD) kukamilisha usimikaji wa mashine za kisasa 10 za kusafisha damu, baada ya hospitali ya rufaa ya Tumbi kuboresha miundombinu ya kuwezesha huduma hiyo kupatikana.
Hatua hiyo ni muendelezo wa maboresho ya huduma za afya nchini yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Afya.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Amani Malima amesema mpaka sasa tayari huduma imeshatolewa kwa wagonjwa watatu na huduma hiyo imefanikiwa kwa asilimia 100.
Kwa upande wake Fundi Sanifu vifaa tiba wa MSD Ikunda Harrison amesema mbali na kufunga mashine hizi MSD ilitoa mafunzo kwa watoa huduma wa hospitali hiyo, ambapo kwa sasa jukumu kubwa la MSD ni kuhakikisha vitendanishi vya mashine hizo vinaendelea kuwepo wakati wote ili kuepuka kukwamisha huduma
- Log in to post comments