Skip to main content
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima Akiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Baadhi ya Viopngozi Mbalimbali wa Srikali na Sekta ya Afya

MSD Yaanza Usambazaji wa Vifaa Tiba kwa Majimbo ya Mkoa wa Morogoro

BOHARI ya Dawa (MSD) imeanza usambazaji majimboni vifaa  tiba  vilivyonunuliwa na serikali vyenye  thamani ya zaidi ya Sh bilioni 14.9 kwa ajili ya hospitali, vituo vya afya na zahanati  lengo ni kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Meneja wa MSD, Kanda ya Dar es salaam, inayohudumia mikoa ya  Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Visiwa vya Zanzibar, Betia Kaema alisema hayo wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , Adam Malima kwa ajili ya majimbo 11 ya Mkoa huo.

Kaema alisema , Mkoa wa Morogoro umepatiwa vifaa tiba vya aina tisa vyenye thamani ya sh milioni 759  na kuanza kusambazwa  katika majimbo yote 11 na  kila jimbo litapokea vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 69.

 “ Kama tunavyofahamu Serikali yetu inayoongozwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan , imenunua vifaa kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na mtoto vyenye thamani ya shilingi bilioni 14.9 na vifaa hivyo vilizinduliwa na Waziri wetu wa Afya  kwa ajili ya majimbo yote Tanzania nzima” alisema Kaema.

Kaema alivitaja  vifaa vilivyokabidhiwa kwa kila jimbo la Mkoa huo  na idadi yake kwenye mabano ni Drip stand  (330), vitanda vya kawaida vya wagonjwa (330), vitanda vya kujifungulia mama wanajawazito (220) na seti (220) za kujifungulia mama wajawazito.

Alitaja vingine ni shuka (1,320), magodoro (330), Examination table (220), meza ndogo za wagonjwa kuwekea vifaa vyao pale wanapokuwa wamelazwa (165) na Bed side Locker (330).

Kaema alisema hizo zote ni juhudi za serikali katika kuondoa kabisa ama kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua  .

“ Kwa sasa serikali imetoa kipaumbele kuimarisha na kuwezesha hospitali zote mikoani ambazo zimeanishwa katika majimbo mbalimbali kuwa  na vifaa hivi ili kuweza kuondokana kabisa na vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua” alisema Kaema .

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima ,alisema serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya sekta ya afya na kwa sasa imejielekeza katika uboreshaji wa viwango vya utoaji wa huduma za afya nchini.

“ Malengo yetu sisi kama mkoa baada ya kupokea kwa vifaa tiba hivi ni kuboresha utoaji wa huduma za afya  kwa wananchi na hili tumekuwa tukilihimiza nyakati zote “ Malima .

Mkuu wa mkoa huyo alisema licha ya kupokea vifaa tiba hivyo, mkakati wa mkoa  huo ni kuendelea kutoa elimu kuhusiana na kujikunga na magonjwa mbalimbali na namna ya utumiaji wa vifaa hivyo kwa wagonjwa.

Hivi karibuni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alizindua usambazaji wa vifaa vya kuboresha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto vyenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 14.9 ambavyo vitasambazwa katika majimbo 214 na halmashauri nchi nzima.

Ummy alisema usambazaji wa vifaa hivyo umelenga kuboresha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto na kuimarisha uzazi salama nchini.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.