Mkurugenzi Mkuu MSD, Abainisha Mafanikio ya MSD Chini ya Awamu ya Sita
DODOMA:
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Mavere Tukai leo tarehe 17/10/2022amekutana na waandishi wa habari Mkoani Dodoma na kutoamrejesho juu ya mafanikio ya Bohari ya Dawa (MSD) chini yaserikali ya awamu ya sita, inayoongozwaMhe. Samia Suluhu Hassan.
Bw. Mavere amesema katika mwaka wa fedha 2022/23,MSD imee ndelea kufanya maboresho ya kiutendaji kamailivyoelekezwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku mabadiliko hayoyakilenga kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afyapamoja na utawala bora.
Amesema serikali ya awamu ya sita kwa mwaka huu wa fedha2022/23, ilitenga shilingi bilioni 200 za ununuzi wa bidhaa za afyanchini ambapo hadi kufikia mwezi huu Oktoba 2022, tayari MSDimepokea shilingi bilioni 57 kwa ajili ya robo mwaka ya kwanza.
Kwa upande wa ununuzi ya bidhaa za afya, MSD imeendelea kuzingatia taratibu, kanuni na sheria, ili kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.
Ameongeza kuwa ununuzi huo unazingatia ubora na thamaniya fedha, ambapo mpaka sasa katika kipindi cha miezi minne MSD imekwisha ingia mikataba hai na ya muda mrefu kwabidhaa zaidi ya 1,000, ili kuharakisha upatikanaji wabidhaa hizo.
Bw. Mavere asema MSD inaendelea na usambazaji wa bidhaaza afya kwenye vituo vyote vya afya vya serikali takribani7,153 kupitia kanda zake 10 zilizowekwa kimkakati, ambapokwa sasa usambazaji huo unafanyika mara sita kwa mwaka,kutoka mara nne za awali.
Aidha kwa upande wa uzalishaji wa bidhaa za afya MSDimeendelea na uzalishaji barakoa, huku mradi wa wa viwandavya Idofi ulioko Makambako uko hatua za mwisho, ambapoukikamilika utazalisha mipira ya mikono (Surgical &Examination Gloves), vidonge (tablets), rangi mbili (capsules),vimiminika (syrup), na dawa za ngozi (ointment & cream).
Miradi hii chini ya MSD itasaidia kuimarisha upatikanajiwa bidhaa za afya nchini.Katika hatua nyingine ameongeza kuwa MSD imeendeleakuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, ili kushiriki katika ujenzi wa viwanda nchinikwa njia ya ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP),ambapo hadi sasa mchakato huo unaenda vizuri, baadaya kukamilika kwa upembuzi yakinifu.
- Log in to post comments