Mhe. Queen Sendiga Aipongeza MSD.
Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Queen Sendiga amefurahishwa na huduma za MSD Mkoani humo na kusema kwamba hivi sasa huduma za afya hasa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba umeimarika kwa kiasi kikubwa.
Mhe. Sendiga ameongeza kuwa huduma na uhusiano wa MSD na Uongozi wa Mkoa wa Rukwa umeimarika na kwamba kero mbalimbali zilizokuwepo hapo awali, mathalani za upungufu wa bidhaa za afya sasa zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa.
“Ukienda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya unakuta dawa muhimu zinapatika kwa kiasi kikubwa, jambo linaloashiria kwamba MSD wameboresha huduma" alisema Sendiga.
Pamoja na kuboreka kwa huduma za MSD, Mkuu huyo wa Mkoa, ameiasa MSD kupitia Meneja wake wa kanda ya Mbeya Ndugu. Marco Masala, kutobweteka, bali kuhakikisha kuwa uboreshaji wa huduma uliopo sasa unakuwa endelevu ili wananchi waendelee kunufaika na huduma za MSD .
Ameongeza kuwa zamani MSD ilikuwa inasemwa sana mitandaoni lakini kwasasa malalamiko yamepungua kwasababu huduma zimeendelea kuwa bora na za kutegemewa.
Kwa upande wake Meneja wa MSD Kanda ya Mbeya, Bw. Marco Masala ameahidi kuendelea kuboresha huduma, na kufanyia kazi changamoto mbalimbali zitazokuwa zikijitokeza ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.
- Log in to post comments