Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Atoa Rai kwa Watumishi wa Afya
Singida.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt.Fatma Mganga, ametoa rai kwa MSD na wataalamu wengine wa afya wakiwemo Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanaboresha huduma kwenye maeneo yao, ikiwemo upatikanaji wa bidhaa za afya, ili kuwahudumia wananchi kwa utimilifu.
Dkt. Mganga ametoa rai hiyo leo, wakati akifungua kikao kazi baina ya MSD na Wadau wake, kilichofanyika Mkoani Singida.
Ameongeza kuwa serikali ya Awamu ya Sita imejenga vituo vingi vipya vya kutolea huduma za afya nchini na kuviongeza hadhi vingine, hivyo kazi kubwa kwa MSD ni kuhakikisha bidhaa za afya hitajika katika vituo hivyo zinapatikana kwa wakati na huduma za afya zinatolewa kwa wananchi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Victoria Ludovick, ameipongeza MSD kwa kuboresha hali ya upatikanaji wa bidhaa za afya Mkoani humo, ambapo kwa sasa umefikia asilimia 88%.
Hata hivyo, ameisihi MSD kuendelea kuboresha upatikanaji huo ili uwe maradufu, mathalani upatikanaji wa vifaa tiba.
Naye Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma. Bw. John Sipendi, amewashukuru wadau hao kwa kuitia mualiko huo, huku akihimiza umuhimu wa mijadala ya wazi ili kupata suluhu ya changamoto mbalimbali na hatimae kutoka na maazimio ambayo yatasaidia kuboresha huduma kwa pande zote mbili.
- Log in to post comments