Skip to main content

Ujumbe wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Watembelea Kanda ya Kilimanjaro

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini MSD Dkt. Ritah Mutagonda, ambaye pia ni mlezi wa MSD Kanda ya Kilimanjaro ameipongeza Kanda ya MSD Kilimanjaro kwa kuvuka lengo la mauzo kwa kufikia 115% katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2024/2025.

Mjumbe huyo wa Bodi ya Wadhamini ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake kwa wateja wanaohudumiwa na Kanda ya Kilimanjaro, kama moja ya shughuli za kuadhimisha miaka 30 ya utendaji wa MSD.

Dkt. Mutagonda pia amemwelekeza Meneja wa Kanda kuhakikisha waaimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya hususani  zile za huduma maalum, ili kuboresha utendaji katika vituo vya kutolea huduma za afya. 

Akizungumza na watumishi wa Kanda ya Kilimanjaro, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa MSD, Jafari Makoka ambaye amefuatana na Mjumbe wa Bodi katika ziara hiyo, amewasisitiza watumishi wa MSD kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, umakini, uaminifu na kufuata sheria na utaratibu.

Ujumbe wa MSD ulitembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi na kuzungumza na uongozi wa hospitali hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine walieleza kuridhishwa na huduma za MSD.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Edna Munisi amewaeleza MSD kuwa wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha jengo la huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo, na tayari imeshapokea baadhi ya mashine kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.

Ziara hiyo imeendelea katika kituo cha afya kilichoongezwa hadhi cha Uru, wilayani Moshi na Zahanati ya Rau iliyopo Manispaa ya Moshi.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.