Skip to main content

Uongozi wa Juu USAID na PEPFAR Watembelea MSD Kanda ya Iringa

Mkurugenzi Mkazi wa USAID Tanzania Craing Hart na Mratibu Mkuu wa PEPFAR Tanzania Jessica Greene wametembelea MSD Kanda ya Iringa kuangalia namna MSD inavyotekeleza Majukumu yake, hasa ununuzi, utunzaji, na usambazaji wa bidhaa za afya zinazofadhiliwa na Mifuko hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo, Bw. Hart na Bi. Greene wameipongeza MSD kwa weledi wake katika usimamizi na usambazaji wa bidhaa za miradi misonge hadi kwa walengwa ambao ni wananchi.

Viongozi hao pia wamepongeza uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Serikali ya Marekani kupitia miradi ya USAID na PEPFAR, huku wakisisitiza kwamba, ushirikiano kupitia miradi hiyo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha na kuimarisha afya za Wananchi.

Katika hatua nyingine wameipongeza MSD kwa kujidhatiti katika adhma yake ya kujiendesha kibiashara, kwani ni hatua nzuri kuelekea uchumi imara na huduma za uhakika.

Aidha, wameahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania, pamoja na wadau mbalimbali ikiwemo MSD, katika nyanja mbalimbali kwa kadri ya mahitaji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bi. Rosemary Slaa ameishukuru serikali ya Marekani kupitia miradi yake kwa kuendelea kuisaidia Tanzania.

Ameongeza kuwa MSD inasambaza bidhaa nyingi zilizoko chini ya wafadhili hao, mathalani bidhaa za UKIMWI, Malaria, pamoja na bidhaa za mama na mtoto.

Rosemary pia amedokeza kwamba MSD imekua mnufaika mkubwa kupitia ujenzi wa maghala, usimikaji mifumo, na ununuzi wa magari ya usambazaji kupitia ufadhali wa wadau hao.

Hata hivyo, ameeleza kwamba bado MSD inakabiliwa na ufinyu wa maghala ya kuhifadhia bidhaa za afya, kutokana na ongezeko la watu, vituo vya afya, zahanati na hospitali nchini, hivyo kuwaomba wadau hao kuendelea kuisaidia MSD, Ili iweze kusimama imara katika mnyororo wa ugavi.

Ziara hiyo imekuja ikiwa ni maadhimisho ya miaka 20 toka kuanzishwa kwa Mfuko wa PEPFAR.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.