Skip to main content
Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai, Akiteta jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA) Bw. Eliakim Maswi,Wakati Alipotembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD) kwa Lengo la Kubadilishana Mawazo.

Mkurugenzi Mkuu MSD, Afanya Mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu PPRA

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Mavere Ali Tukai, amefanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA) Bw. Eliakim C. Maswi, juu ya namna bora ya kuboresha ununuzi wa bidhaa za afya, kufuatia changamoto kadhaa zinazoikabili Bohari ya Dawa kwenye eneo hilo.

Mavere amemuelezea Afisa Mtendaji Mkuu huyo mtazamo wake juu ya ununuzi kwenye nyanja mbalimbali kama vile sheria, taratibu, miongozo pamoja na mfumo wa TANEPS.

 Kupitia kikao hicho Mavere amebainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili Bohari ya Dawa upande wa ununuzi, na namna bora ya kuzitatua, ili kuboresha hali ya upatikanaji wa Dawa na Vifaa tiba nchini.

 Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu PPRA, amempongeza Bw. Mavere kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo, huku akiahidi kufanyia kazi kwa haraka, changamoto mbalimbali za kimanunuzi zinazoikabili MSD.

 Aidha, amesisitiza taasisi za umma zimetofautiana upande wa mahitaji, hivyo kuahidi kuangazia na kutatua changamoto zilizobainishwa ili kuboresha manunuzi ya umma.

About MSD

Medical Stores Department (MSD) was established by the Act of Parliament No.13 of 1993 as an autonomous department under the Ministry of Health, Community Development, Gender, Elderly and Children responsible for developing, maintaining and managing an efficient and cost effective system of procurement, storage and distribution of approved medicines and medical supplies required for use by all public health facilities.