Kamati ya Kudumu ya Bunge ya huduma ya Jamii imetembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa Keko
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya huduma ya Jamii imetembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa Keko na kuipongeza kwa utendaji wake kazi pamoja na mazingira magumu yanayoikabili.Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Peter Serukamba amesema Kamati yake itasimamiana kuyafanyia kazi masuala makubwa manne ambayo ni pamoja na bajeti finyu ya dawa, ulipwaji wa deni la serikali, mfumo wa uwajibikaji kati ya TAMISEMI na Wizara ya Afya ambao unasababisha utekelezaji na usimamizi wa masuala ya Afya kutokuwa na mtiririko kutoka juu kwenda chini. Jambo la nne ni kuhakikisha utekelezaji wa kuongeza uzalishaji dawa ndani ya nchi kupitia sekta binafsi (PPP).