Watumishi wa MSD wapewa mafunzo ya zima moto

Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, mkoa wa Temeke jijini Dar Es Salaam limetoa mafunzo ya zima moto na uokoaji kwa Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) Makao Makuu ambapo pia wamepata elimu ya jumla juu ya uokoaji na kuzima moto kwa vitendo.

Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Zima Moto na Uokoaji, mkoa wa Temeke Castory Willa ameeleza kuwa mara nyingi wananchi wamekuwa hawana uelewa wa kutosha kuhusu kujiokoa pindi wanapopata matatizo ya moto, hivyo ni vyema elimu kama hizi zikazingatiwa na kufanyiwa majaribio mara kwa mara kwa jamii mbalimbali.

Ameongeza kuwa, cha muhimu ni kujua namna ya kujikinga kwanza, kasha kupiga namba maalumu ya huduma ya zima moto ambayo ni 114 mahali popote mtu alipo nchini.Hata hivyo alieleza kuwa ni muhimu kusaini kitabu cha mahudhurio kazini wakati wa kuingia na kutoka kwani ndicho kitu cha kwanza kufuatilia pindi janga linapotokea kwa ajili ya kuokoa watu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Bi. Neema Mwale amesema zoezi hili kisheria linatakiwa kufanyika mara mbili kwa mwaka ili kuhakikisha elimu hii inaeleweka kwa wafanyakazi wote.Mafunzo hayo yalitoa pia fursa ya maswali na majibu, ambapo wafanyakazi walipata fursa ya kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa yanayohusiana na majanga, hasa ya moto.

 

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amezindua duka la dawa la MSD Wilayani Ruangwa

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amezindua duka la dawa la MSD Wilayani Ruangwa, lililopo ndani ya hospitali ya Wilaya hiyo na kuzusema kuwa hiyo ni hatua ya serikali ya kuboresha huduma ya afya kwa kuwawezesha wananchi kupata dawa kwa wakati na kwa bei nafuu.

Amesema duka hilo limewekwa wilayani Ruangwa kwasabu eneo hilo lipo katikati ya wilaya za Liwale, Kilwa na Nachingwea hivyo wananchi wa maeneo hayo na hata mikoa jirani watafaidika na huduma hiyo.

Waziri Mkuu amesema katika mwaka huu wa fedha, serikali imeongeza bajeti ya dawa mara tano zaidi kutoka shilingi Bilioni 29.25 ya mwaka jana hadi Bilioni 251 mwaka huu wa fedha ili kuiwezesha Bohari ya Dawa kujiendesha kwa uhakika zaidi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema MSD sasa ipo katika mchakato wa kununua dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji, ili kuepuka gharama za uagizaji dawa nje ya nchi na uchelewaji wa dawa.

Duka la Ruangwa linafanya maduka ya MSD mpaka sasa kufikia Sita, ikiwa ni pamoja na mengine yaliyopo Arusha, Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam na Chato.

Naye Mfamasia Mkuu wa serikali amesema, hivi sasa wana utaratibu mpya wa kuzipa hadhi hospitali na vituo vya afya kwa kuangalia uwezo wake na ubora wa utoaji huduma, ili kuweza kuzipa madaraja.

 

 

 

 

 

 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (mb), amezindua duka la dawa na maghala matatu ya kuhifadhia dawa ya MSD mkoani Mbeya

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (mb), amezindua duka la dawa la MSD mkoani Mbeya na maghala matatu ya kisasa ya kuhifadhia dawa yaliyopo mkoani Mbeya, Tanga na Tabora.

Mhe. Waziri, ameipongeza MSD kwa kupata maghala matatu ya kisasa pamoja na uanzishwaji wa duka la Mbeya ambalo litasaidia upatikanaji wa dawa kwa wananchi wa Mbeya na mikoa ya karibu. Katika hatua nyingine Mhe. Waziri amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa MSD vibao viwili vya uzinduzi vinavyowakilisha uzinduzi wa maghala ya Tanga na Tabora.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD atoa ufafanuzi kuhusu dawa za shilingi bilioni mbili kuwa njiani kutoka Bohari ya Dawa-keko kwenda Muhimbili

Hivi karibuni vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini vimeripoti taarifa kuhusu dawa za shilingi 2,000,000,000/= (Bilioni Mbili) kuwa njiani kutoka Bohari ya Dawa Keko kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili tangu mwaka 2012.Tunapenda kutoa taarifa kuwa, hakuna dawa ambazo ziko njiani tangu mwaka 2012 kutoka Bohari ya Dawa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali bungeni kuhusiana na hesabu za Hospitali ya Taifa Muhimbili, ilionyesha dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 2.03 havikuwa vimefika Hospitali ya Taifa Muhimbili tangu Mei 2012, licha ya kuonekana kwenye Ankara 23 za Bohari ya Dawa. Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa Ankara hizo sio kwamba dawa hazikufika hospitalini hapo, bali hazikuonekana kwenye vitabu vya kupokelea mali vya Hospitali ya Muhimbili.

 

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi amemkabidhi hati ya kiwanja Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa MSD

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi amemkabidhi hati ya kiwanja Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa MSD Bwana Laurean Bwanakunu,kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Msd kanda ya Dar Es Salaam.

Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi kutoa hati hiyo ya Kiwanja hicho kilichopo eneo la Luguru,wilayani Kinondoni ni itekelezaji wa agizo la Rais,baada ya msd kuonyesha uhitaji wa eneo hilo ili kuondokana na gharama ya kukodisha maghala na majengo ya ofisi kwa Kanda ya Dar Es Salaam.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker