Tangazo la Kuhesabu Mali

Bohari ya Dawa (MSD) inawaarifu wateja wake wote wa Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kuwa; kuanzia tarehe 15/6/2017 mpaka tarehe 30/6/2017 litafanyika zoezi la kuhesabu mali kwa mujibu wa sheria. Kutokana na zoezi hilo la kuhesabu mali, maghala yote ya MSD  yatafungwa kwa kipindi cha wiki mbili kuanzia tarehe 15/6/2017.

Maombi yote ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara yawasilishwe MSD kabla ya tarehe 7/6/2017, ili kukidhi mahitaji wakati wote maghala yetu yatakapokuwa yamefungwa. 

Aidha, huduma ya dharura ya kupata mahitaji itatolewa, pale tu itakapothibitika uhitaji.

MSD yakarabati Ghala la dawa la Mirembe


Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi Jengo la kuhifadhia dawa la Hospitali Maalumu ya Mirembe,Dodoma iliyoifanyia ukarabati wa paa,dari na mfumo wa umeme.Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema inapendeza kwa taasisi za serikali kusaidiana kuboresha huduma na utendaji pale inapowezekana.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean Bwanakunu amesema mbali na ukarabati huo,watoa ushieikiano kuandaa makabati ya kuhifadhia dawa yenye utaalamu unaohitajika.Ameongeza kuwa,Hospitali hiyo itaendelea kuhudumiwa kwa upendeleo,ikiwa ni pamoja na kukopeshwa,kutokana na utofauti wa wagonjwa wanaowahudumia.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Mirembe Erasmus Mndeme ameshukuru kwa msaada huo na kuomba ushirikiano zaidi na MSD,ikiwa ni pamoja na kupata dawa kwa maelewano na kumalizia maeneo ya ndani ya kuhifadhia dawa.

Siku ya wanawake

Wanawake wa MSD waliungana na wanawake wengine duniani kuadhimisha siku ya wanawake, ambapo walitumia siku hiyo kupata mada zinazohusu haiba ya utumishi pamoja na malezi na makuzi ya mtoto. Awali akifungua maadhimisho hayo, mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Dkt. Joseline Kaganda amewapa changamoto wanawake ya kujiendeleza kielimu, ili kuendana na kasi ya maendeleo, sayansi na teknolojia ulimwenguni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD Victoria Elangwa amesema hatua hiyo ya kuwapa mada wanawake imefanywa pia kwenye kanda zote nane (8) za MSD, Mada kuu ilikuwa kudhibiti msongo wa mawazo kazini (stress management at work place) na Kujikinga na magonjwa yanayowasumbua wanawake.

Amesema nia ya mada zote ni kuhakikisha wanawake wanakua na afya bora kimwili na kisaikolojia, ili kuwa imara wawapo kazini na kwenye jamii.Watoa mada walioshiriki siku hiyo ni pamoja na Grace Makani na Ester Simba.

MSD yawahakikishia wawekezaji fursa

 
MSD imeshiriki Jukwaa la Biashara,lililoandaliwa na Kampuni ya magazeti ya TSN,jijini Mwanza. Katika Jukwaa hilo,Msd pia imeshiriki maonesho ya vifaa tiba.
Akiwasilisha mada katika jukwaa hilo Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu amewahakikishia wadau wa Mwanza fursa ya uwekezaji kwenye viwanda vya kuzalisha dawa nchini,endapo watakidhi ubora unaohitajika.
Amesema,hatua hii inafuatia utekelezaji wa sera ya ushirikishwaji wa Sekta binafsi na taasisi za Umma katika uwekezaji.Bwanakunu amefafanua kuwa uanzishwaji wa viwanda nchinni utapunguza gharama za uagizaji dawa na vifaa tiba toka nje ya nchi, kuokoa fedha za kununua nje,kusafirisha,kugomboa na  kupata dawa kwa muda mfupi.
 
 
 

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker