MSD yatunukiwa ithibati ya juu ya ubora ISO 9001:2015
Bohari ya dawa (MSD) imeendelea kukidhi viwango vya ubora vya kimataifa katika mfumo wa ununuzi,utunzaji na usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara (Supply Chain Management) na kupata Ithibati ya Kimataifa ya ubora ya daraja la juu inayojulikana kama ISO 9001:2015 ambayo itadumu kwa miaka mitatu (2018 - 2020).
Hatua hiyo imekuja baada ya ukaguzi wa ubora wa huduma zinazotolewa na MSD uliofanywa na kampuni ya Kimataifa ya ACM LIMITED mwezi Agosti 2017, na kudhihirisha kuwa huduma zake zinafuata miongozo ya ya juu ya kimataifa katika utoaji wa huduma za mnyororo wa ugavi.
Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu amesema kuwa hatua hiyo ya kupata ithibati ya juu ya Ubora ya Kimataifa imethibitisha umahiri wa MSD na imeongeza chachu ya utendaji, ubunifu na kuboresha masuala yote yanayohusiana na mnyororo wa ugavi wa ili kuwapa wananchi huduma bora, zenye viwango, bei kwa nafuu na kuwafikishia kwa wakati.
Bwanakunu ameongeza kuwa Ithibati hiyo inaonesha dhahiri ubora wa mfumo wa ugavi wa MSD kwa wateja na wananchi kwa ujumla, na kueleza kuwa huduma za MSD zinaendelea kuboreshwa zaidi kwani taasisi hiyo iko katika kipindi cha maboresho ya kiutendaji kupitia mpango mkakati wake wa mwaka 2017 - 2020.
Mara ya kwanza MSD ilipata Ithibati ya kimataifa mwaka 2013 (ISO 9001:2008) baada ya kukidhi matakwa ya ubora kwa huduma zake za Ununuzi, Utunzaji na Usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na iliweza kuishikilia ithibati hiyo kwa miaka yote bila kunyanganywa, kutokana na kuonekana kuendelea kukidhi viwango vya ubora kila walipokaguliwa.
Ujumbe kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO
Ujumbe kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) ukiongozwa na Mwakilishi Mkazi (Tanzania) katika Mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele (NTDs) Dkt. Alfoncina Masako Nanai umetembelea Bohari ya Dawa (MSD).
Lengo la ujio wao ni kufuatilia changamoto zinazojitokeza kwenye Mnyororo wa Ugavi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara vya mpango huo (NTDs).
Dawa , vifaa tiba na vitendanishi vya maabara vya Mpango huo vilivyopo kwenye Mnyororo wa Ugavi wa Bohari ya Dawa ni pamoja na Mectizan, Albendazole, Praziquantel na Zithromax.
Pamoja na mambo mengine, ujumbe huo umefurahishwa na mfumo wa usambazaji wa dawa na vifaa tiba unafanywa na MSD pamoja na udhibiti ubora.
Bohari ya Dawa (MSD)imezindua Mpango Mkakati wa Kati 2017 – 2020
Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa dawa na vifaa tiba ukanda wa SADC
Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Africa (SADC) kwa kauli moja wamepitisha uteuzi wa nchi ya Tanzania kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kuwa Mnunuzi Mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya nchi hizo kupitia mfumo wa Ununuzi Shirikishi (SADC Pooled Procurement Services (SPPS).
Uteuzi huo wa nchi ya Tanzania umepita bila kipingamizi mwishoni mwa wiki kwenye Mkutano wa Mkutano wa Mawaziri wa Afya wa nchi za SADC uliowakutanisha Mawaziri wa Afya na Mawaziri wanaohusika na masuala ya UKIMWI uliofanyika mjini Polokwane, Limpopo – Afrika Kusini.
Hatua ya uteuzi wa Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara umetokana na juhudi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa MSD ambapo sasa inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa .
Aidha,umahiri na uzoefu wa Bohari ya Dawa (MSD) katika masuala ya ununuzi, utunzaji na --usambazaji Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara (yaani mnyororo wa ugavi) -unaeleweka na kuaminika vizuri hata na nchi nyingine zilizowahi kututembelea kujifunza na kubadilishana uzoefu.
Kwa hatua hiyo MSD itakuwa na dhamana na majukumu yafuatayo:
$11. Kununua Dawa na Vifaa Tiba kwa ajili ya nchi za SADC
$12. Usimamizi wa taarifa na takwimu za Dawa na Vifaa Tiba vitakavyohitajika
$13. Usimamizi wa kanzidata (Database) ya dawa za nchi wananchama wa SADC na usimamizi wa bei elekezi ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara
$14. Kusimamia manunuzi ya Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya Ukanda wa SADC na kusimamia mnyororo wa ugavi
$15. Kutoa huduma za kitaalamu na kupanga bei elekezi na
$16. Kutoa huduma za ushauri wa kitaalam katika masuala ya dawa na vifaa tiba.
Hatua hii itapunguza kwa kiasi kikubwa bei ya dawa na vifaa tiba kwa ajili ya matumizi ya nchi wananchama wa SADC. Jambo ambalo limeipatia heshima na sifa kubwa Tanzania, kwani imeaminiwa kufanya ununuzi wa dawa kwa niaba ya nchi nyingine kumi na tano (15) ambazo ni wanachama wa SADC.
Tanzania kupewa jukumu hilo ni jambo la kujivunia sana tena inaonyesha dhahiri tumetambulika tuko vizuri kwenye masuala mazima ya mnyororo wa ugavi kwa nchi wanachama wa SADC.
Faida zitakazopatikana kwa Tanzania kuwa Mwenyeji wa huduma hii ni kama zifuatazo:
$11. Heshima kwa nchi yetu kwa kuaminiwa na nchi wanachama wa SADC baada ya kukidhi vigezo vya kitaalam
$12. Viwanda vyetu vya ndani vitaweza kuuza dawa zao kwa nchi za SADC, kwani wajumbe wa mkutano tumekubaliana kuwa na kituo kimoja kitakachoshughulikia udhibiti ubora na ukaguzi
$13. Bei ya dawa itapungua zaidi maana sasa tutaweza kwenda moja kwa moja kwa wazalishaji sio kama nchi (Tanzania), lakini kama Ukanda unaoshughulikia nchi 15
$14. Itaongeza ajira na kuijengea uwezo Bohari ya dawa(MSD)