Dkt. Gwajima, Afanya Ziara MSD
Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo tarehe 3 mwezi wa 7,2021, amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimentiya Bohari ya Dawa (MSD) Kwenye ukumbi wa Bohari ya Dawa ulioko Keko jiji Dar es salaam, lengo likiwa ni kuangalia namna gani ya kuboresha huduma na upatikanaji wa bidhaa za afya nchini.
Dkt. Gwajima licha ya kukutana na Menejimenti ya MSD katika kikao cha ndani, alitembelea kiwanda cha kuzalisha Dawa cha Keko (Keko Pharmaceutical) kilichopo jijini Dar es Salaam, kinachosimamiwa na Bohari ya Dawa (MSD).
Katika Ziara hiyo Dkt.Gwajima alijionea uzalishaji wa dawa ambapo hivi Sasa kinazalisha aina kumi za dawa, zikiwemo za maumivu aina mbili na nyingine 8 zikiwa ni dawa za kuua vimelea vya magonjwa ya kuambukiza (antibacteria/antibiotics). Dkt. Dorothy Gwajima akiwa kwenye kikao cha ndani na Menejimenti ya MSD Hatahivyo, licha ya kazi kubwa iliyofanyika kiwandani hapo, Dkt. Gwajima alitoa maelekezo mbalimbali kwa uongozi wa kiwanda hicho, kwaajili ya kuboresha utendaji, uzalishaji, na taarifa muhimu zinazohusu kiwanda hicho.
Katika hatua nyinine,Dkt. Gwajima alitembelea Maghala ya kuhifadhia dawa, yaliyoko Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), Keko jijini Dar es Salaam, na kuijonea uhifadhi wa dawa, sambamba na changamoto mbalimbali zinazoikumba Bohari hiyo upande wa uhifadhi na kuagiza mabadiliko kwenye maeneo mbalimbali ili kuboresha huduma za usambazaji wa bidhaa za dawa nchini |
Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mej.Gen Gabriel Saul Mhidze