Mkurugenzi Mkuu wa MSD Azunguzia Fursa Zilizopo Katika Soko la Dawa Nchini

95D3F252-9527-491B-96E1-8827461811A4.jpeg

 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean R. Bwanakunu amezungumza na wakufunzi na wanafunzi wa program ya “Industrial Pharmacy” kutoka nchi 8 za Afrika,inayoendeshwa na Chuo Kikuu cha Purdue cha  Marekani kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Arusha na kueleza kuwa maboresho ya kiutendaji yanawezekana pale tu wahusika wote wanapokubali kuwa jukumu hilo linamuhusu kila mmoja.

 

Bwanakunu alizungumza hayo wakati wa kuwasilisha mada juu ya mafanikio ya maboresho ya Kiutendaji ya MSD na Utendaji na uendeshaji wa taasisi za umma.

 

Alizunguzia pia fursa zilizopo katika soko la Dawa nchini,ambapo pamoja na mambo mengine amesema MSD imeboresha maeneo yake mengi ya kiutendaji,kuongeza ufanisi na kumarisha uwezo wa ununuzi ya Dawa.

 

Mkurugenzi Mkuu pia alikuwa mmoja wa wasimamizi washauri wa wanafunzi hao wakati wa uwasilishaji wa mapendekezo yao ya uanzishaji wa viwanda vya kuzalishaji dawa na vifaa tiba nchini Afrika.

 

 

Mkuu wa JKT Atembelea MSD

9140E610-C232-434A-B14E-CC8A7A4EB28E.jpeg

 

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu ametembelea Bohari ya Dawa (MSD) na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw.Laurean R. Bwanakunu  juu ya ushirikiano uliopo kati ya MSD na JKT na namna ya kuboresha ushirikiano huo.

29E855EB-A41C-4EF4-A943-BC92E080BF3E.jpeg

MSD inatumia huduma mbalimbali zinazotolewa na JKT ikiwemo ulinzi kupitia Shirika lake la SUMA JKT na ujenzi wa majengo mbalimbali ya MSD ikiwamo maduka ya dawa ya MSD.

Kwa upande wa MSD inatoa huduma pia kwa JKT zikiwemo dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa ajili ya vituo vya Afya vilivyopo chini ya Jeshi hilo.

Viongozi hao pia wamefanya mazungumzo juu ya ushirikiano wa masuala mengine ya kiutendaji baina ya Taasisi hizi.

MSD Yashinda Tuzo 3 za Mwajiri Bora

ate.jpg

 

 

Bohari ya Dawa (MSD) imeshinda tuzo 3 za Mwajiri bora za ATE kwa mwaka (2018) na kwa mara ya kwanza imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumi bora kwa mwajiri bora Tanzania.

 

atee.jpg

MSD ni kati ya waajiri 59 waliofikia hatua ya mchujo huo na tuzo walizoshinda MSD ni pamoja na Mwajiri Bora anayeangalia USTAWI wa wafanyakazi (employee WELLNESS), Mwajiri Bora wa kizalendo (Overall best local winner) na Mwajiri Bora katika utumishi wa Umma.

ateee.jpg

 

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bi.Victoria Elangwa amesema ushindi huo unatokana na ushirikiano madhubuti kati ya wafanyakazi menejimenti na Wizara, utekelezaji mzuri wa mpango mkakati wa MSD pamoja na mahusiano bora na chama cha wafanyakazi.

 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu amefurahishwa na tuzo hizo na kuwapa rai wafanyakazi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili wapate tija zaidi kama kauli mbiu ya taasisi inavyosema; "Tumedhamiria kuokoa maisha yako".

ateeeee.jpg

 

Tuzo hizo zilitolewa jijini DSM na Waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu Mhe. Jenesta Mhagama.

Mwenyekiti wa Bodi MSD, Aipongenza Menejimenti ya MSD na Wafanyakazi

BARAZA_3.jpg

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Dkt. Fatma Mrisho ameipongeza Menejimenti ya Bohari ya Dawa(MSD) kwa kuboresha hali ya upatikanaji wa dawa kwa wateja wake pamoja na kuimarisha uhusiano mzuri na wadau wake mbalimbali.

 

BAZARA_6.jpg

Dkt.Mrisho amesema hayo alipokuwa akifungua  kikao cha 17 cha Baraza la wafanyakazi la MSD,kinachoendelea mjini  Dodoma.