Ujumbe wa Serikali ya Tanzania Wafanya Mazungumzo na Sekretarieti ya SADC

SADC

Ujumbe wa serikali ya Tanzania, ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki  Ulisubisya ​​​​​​umefanya kikao na uongozi wa juu wa Sekretarieti ya SADC ikiongozwa na Katibu Mtendaji  wake Dkt. Stergomena L. Tax, juu ya utekelezaji wa MSD kununua dawa kwa ajili ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Africa SADC .

 

SADC.3.jpg

 

MSD iliteuliwa kuwa Manunuzi mkuu wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi 16 wanachama   kwenye mkutano wa mawaziri wa Afya wa nchi hizo uliofanyika Novemba mwaka jana(2017) nchini Afrika Kusini.

Katika kikao hicho cha siku mbili, kilichofanyika Gaborone, Botswana pamoja na mambo mengine wamekubaliana  kuwa ili MSD ianze utekelezaji huo, makubaliano kati ya MSD na Sekretariet ya SADC (MoU) inabidi yasainiwe.

 

SADC3.jpg

Kwa mujibu wa Dkt. Ulisubisya makubaliano ya awali yatasainiwa rasmi hivi karibuni. MSD na SADC wameanza  maandalizi  ya utekelezaji wa awali wa mambo waliyokubaliana  kwenye mkutano huo.

Wawekezaji Kutoka China, Watembelea Tanzania

 

Wawekezaji kutoka nchini China, ametembelea nchini Tanzania,ikiwa ni pamoja na kufika Bohari ya Dawa (MSD) kuangalia fursa za uwekezaji kwenye sekta ya viwanda vya dawa na vifaa tiba.


Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu ameeleza kuwa MSD ipo tayari kushirikiana na sekta binafsi kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba nchini na kwamba tayari kuna viwanda vilivyopo China vina mikataba na MSD ya dawa na vifaa tiba.

 

Bwanakunu amewaeleza wageni hao kuwa MSD imeteuliwa kuwa mnunuzi wa Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi vya Maabara kwa ajili ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Ukanda wa Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) hivyo ni fursa nzuri kwao kufanya biashara sasa.

 

 

Aidha Wawekezaji hao kutoka China, walitembelea eneo la MSD, lililotengwa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa viwanda vya dawa nchini, lililoko eneo la Zegereni Mjini Kibaha mkoani Pwani.

Wawekezaji hao walifika na watendaji wa Wizara ya Viwanda na Biashara  kuangalia fursa za uwekezaji  kwenye sekta mbalimbali nchini, ikiwemo sekta ya viwanda vya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.

 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Atiliana Saini Mkataba wa Upimaji Kazi Baina ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vyote vya MSD

 

 

Menejimenti ya MSD leo imeendesha zoezi la kutiliana saini mkataba wa upimaji kazi (Performance Contract) Mkataba huu unatekeleza mpango mkakati wa Bohari ya Dawa (MSD) wa 2017/2020.

Zoezi hili la kutiliana saini limefanyika baina ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean R. Bwanakunu, Wakurugenzi wa Kurugenzi na Wakuu wa Vitengo vyote vya MSD.

Mkataba huu pia hutumika kusimamia na kupima utendaji kazi katika ngazi ya Kurugenzi, Vitengo na mfanyakazi mmoja mmoja ili kuleta tija na ufanisi kiutendaji.

 

 

Bohari ya Dawa (MSD), imefanya mkutano wa mwaka wa wazalishaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara

Bohari ya Dawa (MSD), leo imefanya mkutano wa mwaka wa wazalishaji wa dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara jijini Dar es salaam, wenye lengo la kujadili kwa pamoja juu ya changamoto, maboresho, taratibu na sheria mbalimbali za manunuzi zinazotumika hapa nchini, sambamba na kuwashawishi wazalishaji hao kuja kuwekeza nchini kupitia viwanda vya dawa.Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema MSD imejiimarisha na kujijengea uwezo wa kuwahudumia wateja wake, hivyo inapaswa kuwa na uhakika na upatikanaji wa dawa zenye viwango na ubora unaokubalika.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof.Elisante Ole Gabriel amewahamasisha wazalishaji hao kuchangamkia fursa adhimu ya kuanzisha viwanda vya dawa hapa nchini, kwa kuwa mahitaji ya viwanda vya dawa ni makubwa na kuongeza kuwa, uwepo wa viwanda hivyo utarahisisha upatikanaji wa dawa kwa gharama nafuu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu amesema mkutano huo ni hatua muhimu ya kujadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwa pande zote mbili wakati wa manunuzi ya dawa na vifaa tiba ili kuboresha na kurahisisha mazingira ya kibiashara. Mkutano huo ulioenda pamoja na majadiliano umefanyika ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha ushirikiano na uhusiano wa kibiashara kati ya wadau hao na MSD, ili kuleta tija katika uzalishaji na upatikanaji wa dawa nchini.

Jumla ya wazalishaji 130 kutoka zaidi ya nchi 25 wameshiriki mkutano huo ikiwa ni pamoja na wadau wengine wa MSD.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker