Mameneja wa Kanda za MSD Wanolewa
Mkurugenzi wa Rasilima Watu na Utawala wa MSD, Bw. Erick Mapunda akifungua kikao cha tathimini kilichohusisha Mameneja wa Kanda wa MSD
Mkurugenzi wa Rasilima Watu na Utawala wa MSD, Bw. Erick Mapunda amewataka Mameneja wa Kanda za MSD kusimamia vyema utekelezaji wa majukumu yao ili kufikia lengo la taasisi katika utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.
Bw. Mapunda ametoa rai hiyo leo wakati akifungua kikao kazi cha Memeneja wa Kanda wa MSD waliokutana MSD Makao Makuu kwa ajili ya tathmini ya utendaji ya mwaka wa fedha uliopita, pamoja na kuweka malengo mapya ya mwaka huu wa fedha. Mameneja wa Kanda za MSD, Wakifuatilia mada wakati wa tathimini ya utendaji |