
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Elias Mpedi Magosi (watatu kushoto) na Wajumbe Alioambatana Nao, Wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Bohari ya Dawa (MSD), Mara Baada ya Kutembelea Ofisi za Bohari hiyo, Zilizoko Keko, jijini Dar es Salaam
DAR ES SALAAM:
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Elias Mpedi Magosi
pamoja na ujumbe wake, wametembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), yaliyoko
Keko jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kujionea jinsi taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu
yake sambamba na kupokea mrejesho wa maendeleo ya utekelezaji wa mpango wa
manununzi ya pamoja (SPPS) kwaajili ya nchi wanachana.
Akizungumza kwa niaba ya Menejimenti ya Bohari ya Dawa, Kaimu Mkurgenzi Mkuu
wa Bohari hiyo Bw. Leopold Shayo amempongeza Katibu Mtendaji huyo wa SADC
kwa kuzuru Tanzania, na hasa kuitembelea MSD, huku pia akianisha mafanikio
mbalimbali yaliyopatikana katika Jumuiya hiyo kupitia utekelezaji wa mpango
wa manunuzi ya pamoja kwa nchi wananchama.
Bw. Shayo amesema kwamba hadi kufikia sasa, MSD kupitia manunuzi ya pamoja
kwa nchi za SADC (SPPS) imewezesha kuundwa kwa Miongozo ya SPPS na
Mfumo wa Usimamizi wa mnyororo wa Ugavi kwa nchi wanachama, kuitisha
na kuendesha mkutano wa kitaalamu wa SADC Pooled Procurement wa kikanda
ili kuwezesha kubadilishana taarifa.
Ameongeza kwamba hadi sasa MSD imeweza kutengeneza mfumo kielektroniki
(e-SPPS) ili kusaidia kushughulikia miamala yote ya usimamizi wa ugavi wa
SPPS ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, ambamba na
kuwezesha kusainiwa kwa mikataba 41 na watengenezaji wa bidhaa za afya.
Aidha, Bw. Shayo amesisitiza kwamba MSD imewezesha kukuza uelewa juu
ya matumizi ya mfummo wa SPPS kwa kufanya mikutano na Mabalozi wa SADC
walioidhinishwa na Tanzania na nchi za SADC, ambapo hadi kufikia Februari
2022, nchi tatu (3) Wanachama zilikuwa zimeanza kutumia mfumo wa SPPS,
ambazo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Comoro, na Seychelles huku
zikiokoa kati ya 35% -70% ya gharama za unununzi wa bidhaa za afya.
Katika hatua nyingne nchi tatu (3) zaidi ambazo ni wanachama wa Jumuiya
hiyo ambazo ni Msumbiji, Malawi na Botswana zimeonyesha nia na utayari
wa kutumia jukwaa la SPPS, kutokana na mafanikio yaliyopatikana kupitia
mfumo huo wa manunuzi ya pamoja.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Lojistiki wa MSD, Bw. William Singano, amesema
mbali na mafanikio yaliyopatikana kupitia mfumo huo wa manunuzi ya pamoja,
bado kuna uhitaji wa msukumo kwa nchi wanachama kutumia mfumo huo ili
kuwezesha lengo mahususi la uanzishwaji wa ushirikiano huo kutimia.
Bw. Singano ameuomba uongozi huo wa SADC, kusaidia upatikanaji wa taarifa
za kikanda za wazalishaji wa ndani, walioko ndani ya jumuiya, hatua itayosaidia
kuwawezesha kushiriki katika manunuzi ya bidhaa za afya na kuongeza pato na
ajira kwa nchi wanachama.
Aidha ameuomba uongozi huo wa SADC, kusaidia upatikanaji wa watu
mahususi (conctact person) kutoka nchi wanachama watakao kuwa wakisimamia
mfumo na taarifa zinazohusiana na SPPS. Sambamba na hilo ameuomba uongozi
huo kusaidia upatikanaji wa orodha mahsusi ya bidhaa muhimu za afya 83, pamoja
na wazalishaji ili kusiaidia katika mipango ya manunuzi na uzalishaji.
Kwa upande wake Katibu wa SADC Mhe. Elias Mpedi Magosi ameeleza kuwa
Tanzania kuwa mnunuzi mkuu wa dawa kwa nchi za Ukanda wa SADC ni
heshima kubwa kwa Taifa, kuaminiwa kwa huduma bora, uwezo na kukidhi
vigezo vya kitaalamu katika mnyororo wa ugavi.
Ameupongeza uongozi wa MSD kwa hatua kubwa uliopiga katika mpango
wa manunuzi ya pamoja, huku akiahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali
zilizowasilishwa na MSD, ili kuleta tija na msukumo wa manunuzi ya pamoja ya
bidhaa za afya kwa nchi wanachama.
Hatahivyo; ameitaka MSD kuongeza nguvu na ubunifu ili kuvutia nchi nyingi
zaidi na kuhakikisha kwamba lengo linafikiwa, huku akipongeza mpango wa
kutoa kipaumbele kwa wazalishaji wa ndani, kwani utainua uchumi wa nchi
wanachama pamoja na kuongeza ajira.
|