Usambazaji wa Vifaa vya CEmONC, Mikoa ya Dodoma na Singida

IMG-20220822-WA0119.jpg

             Vifaa vya CEmONC Vikiwa Vimesambazwa na MSD Kwenye Moja ya Kituo

Cha Afya Mkoani Singida.

 

  

DODOMA:

Bohari ya Dawa (MSD), kupitia Kanda yake ya Dodoma inayohudumia Mikoa

ya Singida na Dodoma imeendelea na zoezi la usambazaji wa vifaa vya

huduma ya dharula ya mama na mtoto (Comprehensive Emergency Obstetric

and New Born Care Services – CEmONC). 

 

Akizungumzia usambazaji huo Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma

Ndg. John Sipendi,amesema usambazaji wa vifaa hivyo kwenye

vituo vya kutolea huduma za Afyavinavyohudumiwa na Kanda yake ya

Dodoma ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan

la kuboresha huduma za dharula za mama na mtoto.

 

Amebainisha kwamba kwa sasa Kanda yake inatekeleza usambazaji

kwenye vituo takribani 26 vya kutolea huduma za afya ambavyo

vilianishwa kwa ajili ya kupatiwa vifaa hivyo katika

Mikoa ya Singida na Dodoma.   

 

"Ikumbukwe kwamba Rais amekuwa akiweka wazi kuwa

moja ya vipaumbele katika serikali ya  awamu hii ya 6, ni kuhakikisha

inaboreshaji huduma, hususani zitakazopunguza vifo vya mama na mtoto

wakati wa kujifungua". Alisema Sipendi

 

Meneja Sipendi amesisitiza Kwamba, ataendelea kuhakikisha vifaa vyote

vinavyoletwa kutoka makao makuu vinasambazwa kwa wakati na haraka

kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyoainishwa.

 

Hata hivyo, pamoja na usambazaji wa vifaa vya CEmONC, Kanda ya Dodoma

imeendelea pia na usambazaji bidhaa nyingine za afya kwenye vituo vya kutolea

huduma za afya takribani 685 vilivyopo katika Mikoa ya Singida na Dodoma.

 

Serikali Kuendelea Kuunga Mkono, Ujenzi wa Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba vya MSD.

WhatsApp_Image_2022-08-19_at_20.07.50.jpeg

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Akiongea Mbele ya Wananchi

wa Mji wa Mkambako (Hawapo pichani) Juu ya Hatua Ujenzi wa

Kiwanda cha Dawa na Vifaa Tiba, Wakati wa Ziara ya

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan

Mkoani Njombe

  

 

NJOMBE: 

Serikali imeahidi kuendelea na ujenzi wa Kiwanda cha uzalishaji wa dawa na vifaa tiba

kilichopo chini ya Bohari ya Dawa (MSD), huko Idofi Makambako,

Mkoani Njombe, ilikuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya

nchini sambamba na kuokoa matumizi ya fedha za kigeni.

 

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo, alipokua akitoa

salamu zake kwa wananchi wa Makambako mara baada ya kupewa nafasi ya

kuzungumza kwenye ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa Makambako - Njombe.

 

"Mheshimiwa Rais, hapa Makambako tunajenga kiwanda cha Dawa na Vifaa tiba

ambapo ujenzi wake hapo nyuma ulisimama kwakuwa tunarekebisha mambo

kadhaa, lakini sasa tunaendelea na ujenzi" amesema Waziri Ummy Mwalimu.

 

"Nimesimama hapa kuwahakikishia wana Makambako, serikali itaendeleza

na kukamilisha ujenzi wa kiwanda hiki, na tutaleta shilingi Billioni 17

kukamilisha ujenzi" Alisisitiza Mhe. Ummy Mwalimu.

 

Waziri Ummy amesema hadi sasa serikali imekwisha toa kiasi cha shilingi

Bilioni 18 ikiwa ni kwa ajili ya ujenzi pamoja na kununua baadhi ya mashine

na hadi kukamilika kwake, kiwanda hicho kitagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 35.

 

Aidha Waziri Ummy ameongeza kwamba, kiwanda hicho kitazalisha dawa

za vidonge, (tablets), dawa za maji (syrup), pamoja na mipira ya mikono (gloves),

huku kikitarajia kutoa ajira kwa watu zaidi ya 200.

 

Bohari ya Dawa Msumbiji Yapongeza Juhudi za MSD Kuboresha Huduma, Pamoja na Ujenzi wa Viwanda

WhatsApp_Image_2022-08-19_at_10.10.34_2.jpeg

Wajumbe Kutoka Bohari ya Dawa (CMAM) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (ANARME) Msumbiji, Wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Uongozi wa Bohari ya Dawa (MSD), Mara Baada ya Kutembelea Makao Makuu ya MSD Kwa Lengo la Kubadilishana Uzoefu. 

 

  

DAR ES SALAAM:

Ujumbe kutoka Bohari ya dawa (CMAM) na Mamlaka ya Dawa

na Vifaa Tiba (ANARME) Msumbiji leo wametembelea MSD

Makao Makuu kwa lengo la kujifunza na kubadirishana uzoefu.

 

Ujumbe huo Msumbiji ulifanya ziara ya kutembelea maghala ya kuhifadhia

bidhaaza afya ya MSD pamoja na kiwanda cha kuzalisha barakoa na kiwanda

cha kuzalisha vidonge KPI.

  

Ujumbe huo umevutiwa na hatua ya MSD kuongeza jukumu la kuzalisha

bidhaa za afya ambazo zinasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama

za kuagiza bidhaa hizo kutoka nje.

  

Aidha, pamoja na mambo mengine ujumbe huo ulikutana na Kurugenzi

za Ugavi na TEHAMA na kupata maelezo namna mifumo mbalimbali

inavyofanya kazi katika mnyororo wa ugavi na kuahidi kuiga mazuri punde

tu warejeapo nchini kwao.

 

 Katika hatua nyingine ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea wateja

wa MSD ambao ni hospitali ya Mifupa, MOI na Taasisi ya Moyo (JKCI)

kwa lengo la kujifunza namna taasisi hizo zinavyoendesha shughuli

zake.

 

 

Mhe. Ummy Mwalimu, Azindua Bodi Mpya ya Wadhamini ya MSD.

 

WhatsApp_Image_2022-08-19_at_17.06.42_1.jpeg

Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Akiwa kwenye Picha ya Pamoja na

Wajumbe Wapya wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Mara baada ya

Kuitambulisha Mbele ya Waandishi wa Habari.

 

  

DAR ES SALAAM:

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amezindua Bodi mpya ya Wadhamini ya Bohari

ya Dawa (MSD) na kuwaelekeza wajumbe hao Bodi kuhakikisha wanawezesha kuboresha

upatikanaji wa bidhaa za afya zenye ubora na bei nafuu.

 

Waziri Ummy amewaeleza wajumbe hao wa Bodi ya Wadhamini kuwa watapimwa kwa

kuangalia hali halisi ya upatikanaji wa bidhaa za afya kwenye vituo vya kutolea huduma

za afya nchini.

 

Pia, amewasisitiza kuhakikisha katika majukumu yote ya MSD wanazingatia sheria,

kanuni na taratibu zote za ununuzi wa umma, ili kuleta ufanisi na tija katika utendaji,

sambamba na kuondoa hoja za ukaguzi.

 

WhatsApp_Image_2022-08-19_at_19.33.51.jpeg 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Bi. Rosemary

Silaa amewataka watumishi wa MSD kubadilika na kutekeleza majukumu

yao kwa kuzingatia weledi, ili kubadili taswira iliyojengeka juu ya utendaji

usioridhisha wa taasisi hiyo.

  

Wajumbe hao ni pamoja na Bi.Rosemary Silaa ambaye ni Mwenyekiti, Dkt. Julius Mwaiselage,

Dkt.Ntuli Kapologwe, Meshack Anyingisye, Rehema Katuga, John Mathew Mnali, Dkt. Mwamvita Kissiwa, Dkt. Danstan Hipolite Shewiyo na Brenda Msangi.

 

UNFPA Yatoa Msaada wa Dawa za Uzazi wa Mpango kwa Serikali ya Tanzania

 

WhatsApp_Image_2022-08-19_at_10.10.34_1.jpegUjumbe Maalum Kutoka UNFPA, Ukiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Uongozi wa MSD, Mara Baada ya Kutembelea Makao Makuu ya Bohari ya Dawa, Yaliyoko Keko jijini Dar es Salaam .

 

 

DAR ES SALAAM:

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia Afya ya Uzazi

na Idadi ya Watu UNFPA limeikabidhi Serikali ya Tanzania

msaada wa dawa za uzazi wa mpango.

 

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika Bohari ya Dawa (MSD)

Mwakilishi wa UNFPA nchini Tanzania Bw. Mark Bryan Schreiner

amesema msaada huo ni sehemu ya jitihada za UNFPA kuisaidia

Serikali ya Tanzania kuboresha huduma za uzazi wa mpango

kwa wananchi.

 

Ameongeza kuwa Tanzania imekuwa mshirika mkubwa wa UNFPA

katika utekelezaji na uboreshaji wa huduma za uzazi wa mpango

jambo ambalo linachagiza katika stawisha afya za wananchi

hasa wa hali ya chini.

  

Naye mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Felix Bundala

ameishukuru UNFPA kwa kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo

kati yake na Tanzania hasa katika kuisaidia Tanzania kwenye

nyanja mbalimbali za uboreshaji wa huduma za afya.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai

amesema MSD imepokea dawa hizo na jukumu la MSD ni

kuhakikisha zinafika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya

nchini, lengo likiwa kuboresha huduma za afya hasa ya mama

na mtoto.

 

 

 

 

                                    

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker