MSD yaihudumia hospitali mpya UDOM

Bohari ya Dawa MSD kanda ya Kati, imepeleka dawa na vifaa tiba kwaajili ya Kituo cha Uchunguzi cha Kimataifa cha UDOM UItra Modern Health Institute, kwaajili ya kituo hicho kuanza rasmi huduma baada ya uzinduzi.

Meneja wa MSD Kanda ya Kati Bwana John Sipendi amesema kuwa baada ya kupata maelekezo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kuhusu vifaa tiba na dawa vinavyohitajika walifanya maandalizi na kuvifikisha kituoni hapo mwanzoni mwa wiki hii.

Amevitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni pamoja na mashine za kuwapatia wagonjwa Oksijeni (Oxygen Concentrator), Vifaa vya kujifungulia (Delivery kits), Nguzo za kutundikia dripu (drip stands), mapazia ya kutunzia siri za mgonjwa, (screen folding), mashine za kupimia msukumo wa damu,(BP machines), vifaa vya maabara na dawa muhimu aina 110.

Pia Bohari ya Dawa MSD ipo katika hatua za mwisho za manunuzi ya vifaa tiba (hospital equipments & machines) takribani zaidi ya aina 1,500 kwaajili ya kuimarisha huduma za Kituo hicho cha Uchunguzi cha Kimataifa.

MSD imejipanga na ipo tayari kutoa huduma kwa hospitali na vituo vya afya ili kuboresha afya na kuokoa maisha ya Watanzania ili kuyafikia malengo ya milenia kwa njia ya matokeo makubwa sasa.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker