Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) afurahishwa na utendaji wa Kanda

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu amefanya ziara ya utambulisho kwa wafanyakazi wa MSD wa ofisi za kanda za Mtwara, Mwanza na Kituo cha Mauzo cha Muleba na kusisitiza kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati ya MSD na Halmashauri.

Katika ziara hiyo Bwanakunu aliwatembelea baadhi ya watendaji wakuu wa Mikoa hiyo na Halmashauri ambao ni pamoja na wakuu wa mikoa, waganga wakuu wa mikoa na Wilaya na makatibu tawala wa mikoa, ambapo pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu utaratibu wa usambazaji dawa wa MSD.

Mbali na kukutana na watendaji hao wakuu, Mkurugenzi Mkuu pia alitembelea baadhi ya Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati zinazohudumiwa na MSD ili kupata maoni kutoka kwa walaji kuhusu huduma za MSD.

Katika ziara hizo Mkurugenzi Mkuu alizungumza na wafanyakazi wa kanda na kutembelea maghala ya kuhifadhia dawa ambapo amesisitiza kuboresha mawasiliano na wateja kwa kutoa taarifa muhimu za bidhaa na taratibu za MSD ili kuboresha huduma.

Mkurugenzi Mkuu Bwana Laurean Bwanakunu anaendelea na ziara ya utambulisho kwenye kanda nyingine zilizobaki ambazo ni Moshi, Tabora, Dodoma, Iringa, Mbeya na kituo cha mauzo Tanga.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker