Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Atangaza Neema Sekta ya Afya Nchini

WhatsApp_Image_2022-10-26_at_15.53.56.jpegWaziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Mkurgenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai(wapili kushoto), na Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Togolani Edriss Mavura (wakwanza kulia) Wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Kiongozi wa Serikali ya Jimbo la Chungcheongbuck 

nchini Korea kusini.

  

KOREA KUSINI: 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan

amedhamiria kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa kuwezesha

upatikanaji wa wataalam, dawa, vitendanishi na vifaa tiba.

Mheshimiwa Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Oktoba 26, 2022 baada ya

kushuhudia utiaji saini wa Makubaliano ya Ushirikiano baina ya Bohari

ya Dawa Tanzania (MSD) na Serikali ya Jimbo la Chungcheongbuck

nchini Korea kusini.

 

Akizungumza wakati wa tukio hilo, ambalo pia lilihudhuriwa na Gavana

wa jimbo la Chungcheongbuck, Mheshimiwa Majaliwa amesema “Tukio hili 

la utiaji saini wa makubaliano haya ni ishara kwamba sasa tunakwenda

kuimarika kwenye sekta ya dawa, mkataba huu kwetu ni muhimu kwa

kuwa tunahitaji kujiimarisha katika eneo la upatikanaji wa dawa na tafiti.”

Sehemu ya makubaliano katika mkataba huo ni kujadili na kuendeleza

mahusiano ya kibiashara katika nyanja za masoko ya bidhaa zinazozalishwa

na Makampuni ya dawa katika jimbo hilo.

 

Maeneo mengine ni kubadilishana watumishi, semina za pamoja za wataalamu

wao katika nyanja mbalimbali, kubadilishana na kupeana taarifa za uwekezaji

kwenye sekta ya dawa, msaada wa kitaalamu na wataalam.

 

Mheshimiwa Majaliwa alimueleza Gavana huyo kuwa, kutokana na mpango

wa Serikali wa kuendelea kuimarisha eneo la utoaji huduma za afya, Serikali

ya Tanzania inawakaribisha wawekezaji kwa ajili ya kujenga viwanda vya dawa

na vifaa tiba ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa dawa na vifaa tiba.

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker