Mkurugenzi Mkuu MSD, Abainisha Mafanikio ya MSD Chini ya Awamu ya Sita

WhatsApp_Image_2022-10-17_at_13.24.30.jpeg

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, Bw. Mavere Tukai Akiongea na Vyombo vya Habari Jijini Dodoma, juu ya Mafanikio ya MSD Chini ya Serikali ya Awamu ya Sita.

  

DODOMA: 

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Mavere Tukai leo tarehe 17/10/2022

amekutana na waandishi wa habari Mkoani Dodoma na kutoa

mrejesho juu ya mafanikio ya Bohari ya Dawa (MSD) chini ya

serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa

Mhe. Samia Suluhu Hassan.

 

Bw. Mavere amesema katika mwaka wa fedha 2022/23,

MSD imeendelea kufanya maboresho ya kiutendaji kama

ilivyoelekezwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku mabadiliko hayo

yakilenga kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya

pamoja na utawala bora.

 

Amesema serikali ya awamu ya sita kwa mwaka huu wa fedha

2022/23, ilitenga shilingi bilioni 200 za ununuzi wa bidhaa za afya

nchini ambapo hadi kufikia mwezi huu Oktoba 2022, tayari MSD

imepokea shilingi bilioni 57 kwa ajili ya robo mwaka ya kwanza.

Kwa upande wa ununuzi ya bidhaa za afya, MSD imeendelea

kuzingatia taratibu, kanuni na sheria, ili kuimarisha upatikanaji

wa bidhaa za afya nchini.

 

Ameongeza kuwa ununuzi huo unazingatia ubora na thamani

ya fedha, ambapo mpaka sasa katika kipindi cha miezi minne

MSD imekwisha ingia mikataba hai na ya muda mrefu kwa

bidhaa zaidi ya 1,000, ili kuharakisha upatikanaji wa

bidhaa hizo.

 

Bw. Mavere asema MSD inaendelea na usambazaji wa bidhaa

za afya kwenye vituo vyote vya afya vya serikali takribani

7,153 kupitia kanda zake 10 zilizowekwa kimkakati, ambapo

kwa sasa usambazaji huo unafanyika mara sita kwa mwaka,

kutoka mara nne za awali.

 

Aidha kwa upande wa uzalishaji wa bidhaa za afya MSD

imeendelea na uzalishaji barakoa, huku mradi wa wa viwanda

vya Idofi ulioko Makambako uko hatua za mwisho, ambapo

ukikamilika utazalisha mipira ya mikono (Surgical &

Examination Gloves), vidonge (tablets), rangi mbili (capsules),

vimiminika (syrup), na dawa za ngozi (ointment & cream).

Miradi hii chini ya MSD itasaidia kuimarisha upatikanaji

wa bidhaa za afya nchini.

 

Katika hatua nyingine ameongeza kuwa MSD imeendelea

kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wa ndani na

nje ya nchi, ili kushiriki katika ujenzi wa viwanda nchini

kwa njia ya ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP),

ambapo hadi sasa mchakato huo unaenda vizuri baada

ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker