Tanzania Yapokea Msaada Kutoka Benki ya TDB

WhatsApp_Image_2022-10-14_at_14.11.22.jpeg

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande ( wapili kulia), Akiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe (wa kwanza kushoto), pamoja na Viongozi Wengine Kutoka MSD na Benki ya TDB Wakati wa Makabidhiano ya Msaada wa Vifaa vya Kujikinga dhidi ya UVIKO 19, Uliotolewa na Benki ya TDB.

   

DAR ES SALAAM: 

Serikali ya Tanzania, imepokea msaada wa shilingi milioni 230

kutoka Benki ya Biashara na Maendeleo (TDB) kwa ajili ya

kununulia vifaa vya kujikinga na kupambana na ugonjwa wa Uviko-19.

 

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Uongozi wa benki hiyo Mkurugenzi

wa Uhusiano na Uwekezaji Bi. Mary Kamari, amesema benki yakeimetoa

msaada huo ili kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19,

huku akiahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika

miradi mbalimbali kimkakati ili kuwaletea Watanzania maendeleo.

 

Akipokea msaada huo kwa niaba ya serikali, Naibu Waziri wa Fedha

na Mipango Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), aipongeza benki hiyo

kwa mchago wake kwa sekta ya afya, huku akiisihi kuendelea kushirikiana

na serikali kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo.

 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe

amesema Wizara imepokea msaada huo kwa unyenyekevu mkubwa

kwani utasaidia katika mapambano ya milipuko ya magonjwa yanayoshabihiana

na Uviko-19 mathalani mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, ulizikumba nchi jirani.

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker