Wazalishaji Bidhaa za Afya Kutoka Ucheki, Waitembelea MSD

WhatsApp_Image_2022-10-04_at_11.50.26.jpeg

Wajumbe wa Chama cha Viwanda vya Kuzalisha Bidhaa za Afya Kutoka Jamhuri ya Ucheki (Czech) Wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti ya Bohari ya Dawa (MSD), na Wawakilishi kutoka Wizara ya Afya,Wakati Walipotembelea Makao Mkuu ya Bohari ya Dawa, Keko jijini Dar es Salaam.

  

DAR ES SALAAM: 

Wajumbe wa chama cha viwanda vya kuzalisha bidhaa za afya

kutoka Jamhuri ya Ucheki (Czech) ambao wako ziarani nchini

Tanzania wametembelea Bohari ya Dawa (MSD) na kuelezea

maeneo mbalimbali wanayoweza kushirikiana na Tanzania

hasa upande wa bidhaa afya.

 

Wajumbe hao ambao wamefuatana na Balozi wa Tanzania

nchini Ujerumani ambaye pia anahusika na Jamhuri ya Ucheki (Czech)

Dkt. Abdallah Possi wameeleza kuwa ziara yao nchini Tanzania

ina lengo pia la kuimarisha mahusiano ya kidoplamasia na kuangalia

maeneo ya ushirikiano upande wa bidhaa za Afya ambazo ni pamoja

na dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.

 

Kwa mujibu wa Rais wa Chama hicho Petr Foit, idadi kubwa

ya viwanda nchini mwao imejikita zaidi kuzalisha bidhaa za

afya, hivyo ni vyema wakajua Tanzania ina uhitaji wa bidhaa

za aina gani ili kuweza kushirikiana katika hilo.

 

Ujio huo pia umeonesha nia ya kuipatia Tanzania bidhaa za

kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwa ni pamoja na Ebola,

ambapo Wizara ya Afya kupitia MSD watakaa na kuainisha

mahitaji hayo,na kuwasilisha kwa Rais wa Umoja huo wa

wazalishaji ili kufanya utaratibu wa kupata bidhaa

walizonazo.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker