Serikali Ya Misri Yatoa Msaada wa Vifaa Tiba kwa Tanzania

WhatsApp_Image_2022-09-19_at_13.50.42.jpegBalozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abuwafa (Kulia) Akikabidhi Msaada wa Vifaa Tiba kwa Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daudi Msasi(Kushoto), Makao Makuu ya Bohari ya Dawa, Jijini Dar es Salaam.

  

DAR ES SALAAM: 

Ubalozi wa Misri nchini Tanzania, leo tarehe 8/9/2022, umetoa

msaada vifaa tiba kwa Serikali ya Tanzania, kwa ajili ya kuboresha

huduma za afya nchini.

 

Vifaa hivyo vyenye thamani ya dola za Kimarekeni elfu 27 (USD 27,000),

ambazo ni sawa na takribani shilingi milioni 62.9 za kitanzania, umekabidhiwa

rasmi kwa serikali ya Tanzania.

 

Akikabidhi msaada huo Balozi wa Misri hapa nchini,

Mhe. Mohamed Gaber Abuwafa amesema serikali ya Misiri

itaendelea na juhudi za kuunga mkono serikali ya Tanzania

kuboresha huduma za afya.

 

"Serikali ya Misri kupitia shirika lake la EAPD, imetoa msaada huu

ili kuboresha huduma za afya, ikumbukwe huu sio msaada wa

kwanza na wala hautakua wa mwisho, kwani nchi zetu zimekua

na uhusiano wa muda mrefu katika nyanja mbalimbali,

hivyo mbali na msaada huu, tunatazamia siku zijazo

kuazisha ushirikiano katika kubadilishana utaalamu na

wataalamu kupitia sekta ya afya".

Alisisitiza Balozi Mhe. Abuwafa

 

Mhe. Abuwafa ameongeza kuwa Serikali ya Misri inaangalia

uwezekano wa kuwekeza nchini kwenye sekta ya viwanda

vya dawa na vifaa tiba, ili kuendeleza uhusiano wa muda

mrefu baina pande hizo mbili.

 

"Serikali ya Misri itaendela kusaidia sekta mbalimbali nchini,

ikiwemo uanzishaji wa viwanda vya dawa, ili kuunga mkono

juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha na

kusogeza huduma za afya karibu na jamiii kwa gharama nafuu"

Alisema Balozi Abuwafa.

 

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania,

Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi, ameishukuru Serikali

ya Misri kupitia ubalozi wake nchini, kwa kuipatia Tanzania

msaada huo, na kusisitiza kwamba utaenda kuwa chachu ya

kuboresha afya za wananchi.

 

"Kwa niaba ya serikali ya Tanzania, tunaipongeza na kuishukuru

serikali ya Misri kwa kutupatia msaada huu kwaajili ya kuboresha

afya za watanzania na ushirikiano uliopo baina ya mataifa yetu,

tunatumaini kwamba huu hautakuwa msaada wa mwisho,

bali muendelezo wa ushirikiano zaidi baina ya mataifa yetu."

Alisema Msasi

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker