MSD Yatoa Mafunzo kwa Wataalamu wa Vifaa Tiba na Maabara Nchini.

WhatsApp_Image_2022-09-19_at_13.26.53.jpegKaimu Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji wa MSD Bw.William Singano, Akiongea na Wataalamu wa Vifaa Tiba na Mabaara nchini, Wakati wa Kufunga Mafunzo, yaliyoendeshwa na MSD kwa Wataalamu Mkoani Morogoro.

  

Morogoro: 

Mafunzo ya siku tatu kwa wahandisi vifaa tiba na wataalam wa Maabara

nchini, yamefungwa leo mkoani Morogoro.

 

Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa wakati mmoja kwa mikoa mitano kwa ajili ya wataalam

wa nchi nzima yalikuwa na lengo la kuwafundisha wataalamu wa usimikaji,

matumizi na ukarabati wa mashine za maabara na vifaa vinavyosambazwa

na MSD.

 

Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD,

Kaimu Mkurugenzi wa Ugavi na Uendeshaji Bw.William Singano amesema

mafunzo hayo ni muhimu kwa wahandisi vifaa tiba na wataalam wa maabara

kwa kuwa yanawawesha watumiaji hao kumudu kuzitumia, kuzitunza na

kuzifanyia ukarabati.

 

BW. Singano ameishuikuru Serikali kuboresha huduma za afya kwa kuwezesha

mashine na vifaa vya kisasa nchi nzima.

 

Mafunzo hayo yalitolewa mikoa ya Tabora, Morogoro, Mbeya, Kilimanjaro

na Mwanza ambapo wataalam kutoka mikoa mingine yote waliungana

kupata mafunzo hayo kwa pamoja.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker