Dkt. Mollel Aishauri MSD Namna ya Kuboresha Upatikanaji wa Bidhaa za Afya Nchini.

WhatsApp_Image_2022-09-01_at_08.10.55.jpegNaibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel Akiongea Watumishi wa MSD, Mara baada ya Kutembelea Banda lao, Wakati Maonesho ya Kimataifa ya Wadau wa Bidhaa za Afya ya Afrika Mashariki, Yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.

 

 

  

DAR ES SALAAM: 

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameishauri Bohari ya Dawa (MSD)

kutengeneza mpango wa muda mrefu wa kuzungumza na wazalishaji dawa

na bidhaa nyingine za afya kutoka nchi zinazozalisha bidhaa hizo, ili

kuja kuwekeza nchini Tanzania, hatua ambayo itarahisisha upatikanaji

wa bidhaa za afya nchini.

 

 

Naibu waziri ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa maonesho ya

Kimataifa ya wadau wa bidhaa za afya ya Afrika Mashariki

yaliyoanza leo jijini Dar es Salaam.

 

 

Ameongeza kuwa MSD pia iangalie namna ya kuingia mikataba na nchi

zinazozalisha bidhaa za afya kurahisisha kununua moja kwa moja kutoka

kwao, ili kupunguza gharama na kuwezesha kupata bidhaa za

kutosheleza mahitaji.

 

 

Kiongozi huyo pia amewahimiza wazalishaji hao wa nje kuja kuwekeza nchini

Tanzania kwa kuingia ubia na serikali.

 

 

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano MSD Bi. Etty Kusiluka,

 amemshukuru Dkt. Mollel kwa ushauri, na kuahidi kuufikisha kwenye Menejimenti ya

MSD ili uweze kufanyiwa kazi.

 

 

Aidha, ameendelea kuwakaribisha wananchi na wadau mbalimbali kutembelea banda la

MSD lilipo kwenye maonyesho hayo, ili waweze kupata taarifa mbalimbali

zinazohusiana na MSD, sambamba na kufahamu namna taasisi hiyo

inavyotekeleza majukumu yake.

 

 

Maonyesho hayo ya Kimataifa ya bidhaa za afya ya Afrika Mashariki yanafanyika

kwa siku tatu katika ukumbi wa Diamond Jubilee, ulioko jijini Dar es Salaam,

kwa kuwakutanisha Wadau kutoka nchi mbalimbali.

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker