MSD Yachangia Maboresho ya Huduma za Uzazi Visiwani Zanzibar

WhatsApp_Image_2022-08-30_at_09.45.30.jpeg

Kaimu Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam Bw. Nuru Mwagoka,Akipokea Cheti Kutoka Kwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar     Mhe. Dkt. Husein Ally Mwinyi Kufuatia Mchango MSD Kwenye Mbio za Hisani Zilizolenga Kuboresha Huduma za Uzazi

 

  

ZANZIBAR:

Bohari ya Dawa (MSD), imeshiriki mbio na matembezi
ya hisani kwa ajili kuchangia huduma za uzazi salama kwa mama
na mtoto, zilizoandaliwa na Shirika la AMREF,
visiwani Zanzibar.
 
Akizungumza wakati wa kuhitimisha mbio hizo zilizoanzia
viwanja wa Maisara- Mnazi Mmoja majira ya asubuhi,
Mgeni Rasmi wa Shughuli hiyo, Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Dkt. Husein Ally Mwinyi,
amewapongeza washiriki wote ikiwemo MSD kwa kushiriki
tukio hilo la kihistoria kuchangia maboresho ya huduma za
uzazi salama visiwani humo.
 
WhatsApp_Image_2022-08-30_at_09.45.29.jpeg 
“Nawapongeza wananchi, makampuni na mashirika wote
kwa ujumla kwa kushiriki kwenu kwenye mbio hizi za kusaidia
huduma ya mama na mtoto". Alisema Dkt. Mwinyi. 
 
Rais Mwinyi ametoa wito kwa taasisi, makampuni na wadau
mbalimbali kuiga mfano wa AMREF, ili kusaidia huduma
mbalimbali visiwani humo.
 
Ameongeza kwamba Serikali yake itaendelea kushirikiana
kwa ukaribu na wadau wote wenye nia ya kuchangia
maendeleo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Kaimu
Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam, Bw. Nuru Mwangoka,
amesema MSD ni mdau wa karibu kwa serikali ya mapinduzi
ya Zanzibar hasa kupitia sekta ya afya, hivyo walivyopokea
wito wa kushiriki na kuchangia huduma za afya hawakusita
kufanya hivyo.
WhatsApp_Image_2022-08-30_at_09.45.301.jpeg
 
"Sisi MSD, ni washirika muhimu wa sekta ya afya Zanzibar
kwani tumekua tukifanya kazi zetu kwa ushirikiano na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, hivyo tulivyopokea wito wa
kushangia huduma hizi za uzazi hatukusita kushiriki”
alieleza Bw. Mwangoka
 
Aliongeza kuwa MSD kwenye mbio na matembezi hayo ya hisani,
imeweza kuchangia vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha
huduma za uzazi salama, visiwani humo.
 
Aidha, amesema msaada huo umekwisha wasilishwa kwa uongozi
wa AMREF, ukisubiri kupelekwa kwenye vituo vya kutolea
huduma za afya.
 
Katika mbio na matembezi hayo, washiriki wote wameweza
kutembea na kukimbia mbio hizo na kumaliza ikiwemo Kilometa 5,
na Kilometa 10, ambapo zote zimemalizikia katika viunga
vya uwanja wa Amaani.

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker