MSD Yapongezwa kwa Mageuzi ya Huduma, ndani ya Muda Mfupi.

WhatsApp_Image_2022-08-19_at_10.10.34.jpegMganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora mkoani Tanga, Dkt.Angelina Meshack, Akiongea na Waandishi na Ujumbe Maalum Kutoka MSD (Hawapo Pichani) Walipomtembelea Ofisini Kwake, Kupata Mrejesho wa Huduma Zitolewazo na Bohari ya Dawa (MSD)

 

TANGA:

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makorora mkoani Tanga, Dkt.Angelina Meshack

ameipongeza serikali kupitia MSD, baada ya kupokea vifaa vya chumba cha

upasuaji ikiwemo kitanda cha upasuaji, mashine ya dawa ya usingizi na taa

zinazotumika wakati wa upasuaji amesema vifaa hivyo ni msaada mkubwa

katika kituo hicho kwani awali kulikuwa na changamoto kwenye hutoaji huduma.

 

"Awali tulikuwa hatufanyi upasuaji kabisa kwa hiyo tulivyopokea fedha

kwa ajili ya ukarabati majengo ya kufanyia upasuaji tulifanya hivyo na

baadae vifaa vililetwa na MSD na kuanza kutoa huduma za upasuaji".

Amesema Dkt.Angelina

 

Amesema baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo walianza kutoa huduma ya

upasuaji mbalimbali wa mama wajawazito pamoja na upasuaji mdogo

kwani hapo awali walikuwa wanawapeleka wagonjwa hospitali ya Bombo

kwa sababu huduma hiyo haikuwepo hapo kituoni."Kwa ujio wa vifaa hivi imerahisisha mama mjamzito akipata changamoto

moja kwa moja tunaweza kumpa huduma ya upasuaji na tunaokoa

maisha ya mama pamoja na kichanga". Amesema.

 

Pamoja na hayo Dkt.Angelina amesema walikabidhiwa pia na jenereta kwa ajili

ya hospitali hiyo lakini wakaamua kuwasiliana na ofisi ya mganga mkuu ili

waweze kuichukua na kuikabidhi kwenye vituo vingine ambavyo havina jenerata

kwa sababu kituo hicho kilikuwa na jenerata ambayo walikuwa wameshanunua awali.

 

Ameeleza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa katika kituo hicho ni nzuri kwani

kwa sasa dawa muhimu zinapatikana kwa asilimia 90 na wanaendelea kutoa

huduma bora kwa wananchi

                                    

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker