Kamati ya Afya Bunge la Zambia, Yaipongeza MSD kwa Maboresho ya Utendaji na Ujenzi wa Viwanda

WhatsApp_Image_2022-08-19_at_14.21.00.jpeg

Kamati ya Bunge ya Afya, Maendeleo na Huduma za Jamii ya Bunge la Zambia Ikiwa kwenye Ziara ya Kutembelea Viwanda vya MSD.

 

 DAR ES SALAAM:

Kamati ya Bunge ya Afya, Maendeleo na Huduma za Jamii,ya Bunge la Zambia

wamevutiwa na hatua ya Bohari ya dawa (MSD) kuanza kuzalisha baadhi ya

bidhaa za afya kwa kutumia wataalam wake wa ndani.

Hayo yamebainishwa hii leo, tarehe 26/5/2022 baada ya Kamati hiyo ya Afya

kutoka Zambia, kuitembelea MSD kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu

katika masuala yanayohusu mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.

WhatsApp_Image_2022-08-19_at_14.20.28.jpeg

Akizungumza kwaniaba ya ujumbe huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge ya Afya,

Maendeleo na Huduma za Jamii, ya Bunge la Zambia, Mhe.Dkt. Christopher K. Kalila

amesema wamevutiwa na hatua ya Bohari ya dawa (MSD) kuanza kuzalisha baadhi

ya bidhaa za afya kwa kutumia wataalam wake wa ndani.

 

Mhe.Dkt. Kalila ameongeza kuwa MSD Tanzania ni kama pacha wa Bohari ya Dawa

ya nchini Zambia, kwani sheria yao pia imefanyiwa mabadiliko na kuiwezesha Bohari

hiyo kuanza kuzalisha bidhaa za afya.

 

"Ni vyema taasisi zetu hizi mbili zikawa karibu ili kubadilishana uzoefu, na utaalamu

katika maeneo mabalimbali ili kusukuma kwa pamoja ajenda ya uanzishaji wa viwanda

vya bidhaa za afya na kuondoa utegemezi wa bidhaa kutoka nje sambamba na kupunguza

gharama." Alisema Dkt. Kalila.

WhatsApp_Image_2022-08-19_at_14.20.27.jpeg

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai amesema

kwa pamoja na nchi nyingine kama Zambia yanaweza kufanyika mazungumzo

ya pamoja ya kuwezesha ununuzi wa pamoja wa bidhaa za afya, kupitia mpango

wa manunuzi ya pamoja ya SADC unaoratibiwa na MSD kwa nchi 16, kwa

kupitia mpango huo, nchi wanachama zitanufaika, sambamba na kupaisha soko

la viwanda vya ndani.

 

Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na mambo mengine wametembelea viwanda vya

MSD vya kuzalisha barakoa, pamoja na kiwanda cha dawa cha Keko Pharmaceuticals,

kinachosimamiwa na MSD.

                                              

 

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker