Mkurugenzi Mkuu MSD, Awafunda Wataalamu Sekta ya Afya

DG-3.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze, Akihutubia Wakati wa Kikao Kazi Kati ya MSD na Wataalamu wa Maabara, Mafundi Sanifu na Wahandisi Vifaa Tiba Kutoka MSD, Halmashauri na Hospitali Mbalimbali Nchini

                                       

                     Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Saul

                         Mhidze amesema kuwa na wataalam wa ndani

                   wanaomudu kutumia vifaa vya maabara na kuvikarabati

                       wenyewe ni hatua nzuri itakayopunguza gharama.

 

                         Ameyasema hayo alipozungumza na Wataalamu

                         wa maabara, Mafundi Sanifu na Wahandisi vifaa

                     tiba kutoka MSD,Halmashauri na Hospitali mbalimbali

                      nchini, ambao wapo kwenye mafunzo ya namna ya

                         kufunga, kutumia na kuzifanyia matengenezo

                  mashine mbalimbali za maabara  ambazo zinatarajiwa

                                           kufungwa nchi nzima.

 

                         Mashine hizo za maabara zitapunguza gharama

                         za vipimo vya uchunguzi wa magonjwa kwa zaidi

                                            ya asilimia hamsini.

 

DG-2.jpg

Wataalamu wa Maabara, Mafundi Sanifu na Wahandisi Vifaa Tiba Kutoka MSD, Halmashauri na Hospitali Mbalimbali Nchini, Wakiwa Kwenye Mafunzo Mkoani Morogoro

                              

                                              

DG-1.jpg

Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Saul Mhidze, Akichagiza Mada Wakati wa Kikao Kazi Kati ya MSD na Wataalamu wa Maabara, Mafundi Sanifu na Wahandisi Vifaa Tiba Kutoka MSD, Halmashauri na Hospitali Mbalimbali Nchini

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker