MSD,Waganga Wakuu Mikoa na Wilaya Wajadili Upatikanaji Dawa Nchini

msasi_1.jpg

Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi, Akihutubia Wakati wa Kikao Kazi Kati ya MSD na Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya Kilichofanyika Mkoani Dodoma.

           

                                         Mfamasia Mkuu wa Serikali Daud Msasi amewashauri 

                                         Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuunga Mkono

                                         juhudi za MSD kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya

                                    maabara, hatua ambayo itapunguza gharama za matibabu.

 

                                     Msasi amesema hayo kwenye kikao kazi cha MSD  na

                                   Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya uliofanyika Mkoani

                                                                      Dodoma.

 

                                Pia amewashauri MSD kuendeleza vikao vya aina hii kikanda,

                                  ili kujadiliana kwa kina namna ya kuboresha huduma, kwa

                                kuwa vikao hivi vinawakutanisha wataalamu mbalimbali ikiwa

                                     ni pamoja na wafamasia na wataalamu wa maabara.

msasi_3.jpg

Baadhi ya Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya Wakisilikiza Mada, Wakati wa Kikao Kazi Kati Yao na MSD Kilichofanyika Mkoani Dodoma.                              

                              

                               Kwa upande wake mwakilishi wa Waganga wakuu wa mikoa

                              Dkt. Japhet Simeo amewashauri waganga wakuu wa mikoa na

                                wilaya kutoa ushirikiano wa karibu kwa MSD ili kuboresha

                                                mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.

 

 

 

                                 Amesema wakati huu ambapo MSD imekuja na mikakati

                                    mipya ya kuzalisha dawa na vifaa tiba ili kuwezesha

                                kupunguza gharama za bidhaa za afya, wao kama wataalam

                                            wawe washauri na waunge mkono juhudi hizo.

washima.jpg

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD Ndugu. James Washima, Akihutubia kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Wakati wa Kikao Kazi Kati ya MSD na Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya Kilichofanyika Mkoani Dodoma.

                                   

                                   Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MSD 

                                     Ndugu James Washima amesema kupitia Mkutano

                                      huu MSD inategemea kupata mrejesho mkubwa

                                        wa huduma inazozitoa kwa vituo vya kutolea

                                                     huduma za afya nchini.

 

 

 

 

                                                       “Tunawahakikishia kuwa

                                         tutachukua ushauri, maoni na changamoto

                                   mtakazotupatia na kuzifanyia kazi”. Alisema Washima

 

                         Amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa MSD Meja Jenerali Gabriel Mhidze

                        na watendaji wote wa MSD  kwa maono yao ya kuanzisha viwanda vya

                        kuzalisha dawa na vifaa tiba kwani ununuzi bidhaa hizo kutoka nje ya nchi

                      na kwingineko  umekuwa ukiigharimu serikali fedha nyingi ambazo zingeweza

                                                   kutumika kuboresha huduma nyingine.

msasi_2.jpg

Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya Wakifuatilia Mada Wakati wa Kikao Kazi, Kati Yao na MSD Kilichofanyika Mkoani Dodoma.


                    

 

                          “Kamati yetu imesikia changamoto kutoka kwenu zinazowakwamisha kusonga

                          mbele, tunazichukua na kuzifikisha serikalini ili kuhakikisha MSD inaimarika

                            ipasavyo ili kuwezesha upatikanaji wa dawa nchini".Alisisitiza Washima

 


               

Lock full review www.8betting.co.uk 888 Bookmaker